Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna
Makinda akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamko la kutogombea
Uspika Msimu huu hawapo pichani katika mkutano wake uliofanyika leo
jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo anayotoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda hayupo pichani alipotoa tamko la kutogombea tena Uspika wa Bunge msimu huu.
Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo anayotoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda hayupo pichani alipotoa tamko la kutogombea tena Uspika wa Bunge msimu huu.
Spika wa bunge la Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda katikati akiwa katika picha ya
pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wake katika
ofisi za bunge leo jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakifatilia
kwa makini maelezo anayotoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Anna Makinda hayupo pichani alipotoa tamko la kutogombea
tena Uspika wa Bunge msimu huu.
…………………………………………………………………………………….
Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO-Dar es salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda ametangaza rasmi kutogombea
nafasi ya Uspika wa Bunge baada ya kuliongoza Bunge la 10 kwa kipindi
cha miaka mitano.
Mhe.Makinda ametoa kauli hiyo
leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizingumza na waandishi wa
habari katika ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
“Kama yalivyo matakwa ya
kisheria na demokrasia ya hapa nchini wanasiasa wanatumikia nafasi zao
mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitano na kisha wanarudi kuomba tena
ridhaa kwa wananchi kuongoza”,alisema Mhe.Makinda.
Mheshimiwa Makinda aliongeza
kuwa anaona wakati umewadia kwa yeye kuwaachia wengine nao washike
wadhifa huo katika Mhimili huo muhimu wa kusimamia Serikali.
Mbali na hayo Mhe.Makinda
aliendelea kusema kuwa ametumikia nafasi mbalimbali katika Siasa kwa
kipindi cha miaka 40 ndani ya Bunge, ikiwemo nafasi ya Waziri
,Mwenyekiti wa Bunge,Naibu Spika na Spika hivyo kwa sasa ameamua
kung’atuka katika masuala ya uongozi.
Hata hivyo Mheshimiwa Spika
amewaambia waandishi wa habari kuwa katika kipindi cha uongozi wake,
Bunge lilifanyakazi kwa ushirikiano na liliweza kuisimamia Serikali hadi
kupelekea baadhi ya Mawaziri kujiuzulu.
Ameongeza kuwa Bunge la 10
lilifanikiwa kubadilisha mfumo wa bajeti kwa kuweka sheria mpya za
bajeti ambayo iliongeza nidhamu katika matumizi ya fedha.
Mheshimiwa Makinda amesema kuwa
atawakumbuka Waheshimiwa mbalimbali katika bunge aliloliongoza akiwemo
Mhe.Tundu Lissu , Mhe.Halima Mdee, Mhe.Felix Mkosamali,Mhe.Moses
Machali,Mhe. John Mnyika na wengine ambao alifanya nao kazi kwa
kushirikiano.
Tags
HABARI KITAIFA


