Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo
wakati wa ibada ya msiba ya mjukuu wake marehemu Maryfaustina Yose
Mlyambina(8) iliyofanyika huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo
na Mwili wa Marehemu umesafirishwa kwenda Magu kwa mazishi.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janet Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza la mjukuu wao marehemu Maryfaustina Yose Mlyambina(8) wakati wa ibada ya msiba iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu Temboni Kimara jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwafariji wazazi wa Marehemu Jose Mlyambila na Suzan wakati wa ibada ya mazishi ya mjukuu wake marehemu Maryfaustina Yose Mlambila huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janet Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza la mjukuu wao marehemu Maryfaustina Yose Mlyambina(8) wakati wa ibada ya msiba iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu Temboni Kimara jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu awamu ya Nne
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za
mwisho mbele ya jeneza la mjukuu wa Rais John Pombe Magufuli marehemu
Maryfaustina Yose Mlyambina aliyefariki akiwa na umri wa miaka nane
baada ya kuugua.Ibada misa ya kuuombea marehenu na kutoa heshima za
mwisho zilizofanyika nyumbani kwa wazazi wa Marehemu huko Temboni Kimara
jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janet Magufuli(wapili
kulia), Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassani Suluhu(wapili kushoto), Rais
Mstaafu awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma
Kikwete pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Said Meck Sadik
wakiwa katika ibada ya kuuombea marehemu mjukuu wa Rais John Pombe
Magufuli marehemu Maryfaustina Yose Mlyambila iliyofanyika nyumbani kwa
wazazi ya marehemu Kimara Temboni jijini Dar es Salaam leoRais Dkt.John Pombe Magufuli akiwafariji wazazi wa Marehemu Jose Mlyambila na Suzan wakati wa ibada ya mazishi ya mjukuu wake marehemu Maryfaustina Yose Mlambila huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo.
Tags
HABARI KITAIFA





