Beatrice Lyimo
Dar es Salaam
Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu
wa Serikali imeandaa warsha ya mafunzo juu ya kujiandaa kukabiliana na
dharura ya kemikali hatari na zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye
maeneo ya bandari.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa
mkemia mkuu wa serikali Prof. Samweli Manyele amasema kuwa lengo la
warsha ya mafunzo hayo ni kuwasilisha na kusambaza matokeo ya utafiti
kwa kuhamasisha matumisi salama ya kemikali katika ukanda wa afrika.
“kufundisha nchi za ukanda wa
Afrika Mashariki juu ya namna ya kushughulika na kusimamia kemikali
hatari na zenye madhara, namna ya kujiandaa na kukabiliana na matukio ya
kemikali pamoja na kubadilisha uzoefu wa ushughulikiaji salama wa
kemikali hizo kati ya nchi na nchi” aliongeza Prof Manyele.
Pia kujadili mahitaji ya nchi na
kikanda pamoja na kutambua hatua za kuelekea njia bora Zaidi ya
kujianda na kukabiliana na matukio ya kemikali katika maeneo ya bandari
na njia za usafirishaji ni moja ya lengo ya warsha hiyo.
“Ni matumaini yangu warsha ya
mafunzo hayo yatakuwa muhimu katika kuongeza uelewa wa washiriki na
kujenga uwezo wao wa kushughulikia mizigo ya kemikali hatari kwa usalama
na hivyo kulinda afya, mazingira na mali dhidi ya madhara ya kemikali
hizo” alifafanua Prof. Manyele.
Warsha hiyo itafanyika kwa muda
siku mbili kuanzia tarehe 26 hadi 27 Noverma, 2015 kwenye ukumbi wa
Protea Courtyard Hotel iliyopo jijini dar es salaam na kuhusisha nchi
mbalimbali.
Tags
HABARI KITAIFA