Serikali imewataka wachambuaji na
wasambazaji wa mbegu za pamba kuacha kuwasambazia wakulima mbegu
zilizozalishwa katika maeneo yaliyobainika kuwa na ugonjwa wa mnyauko
fusari (Fusarium Wilt Disease). Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi
wa Huduma za Usimamizi, Bodi ya Pamba Tanzania, Bwana James Shimbe.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari, Bwana Shimbe amesema, ugonjwa wa mnyauko fusari unaweza
kudhibitiwa ikiwa wakulima wa pamba watatumia mbegu bora kutoka kwa
wasambazaji wanaotambulika na Bodi ya Pamba Tanzania.
Akizungumzia tatizo la kuenea kwa
ugonjwa huo Bwana Shimbe amesema kwa kiasi fulani limetokana na baadhi
ya wachambuaji wasio waaminifu kuendelea kusambaza mbegu za pamba za
kupanda ambazo zinaweza kuwa zimetoka katika maeneo yaliyobainika kuwa
na ugonjwa wa mnyauko fusari.
“Tulishatoa maelekezo kwa kuwataka
wasambazaji wa mbegu za pamba za kupanda kutosambaza mbegu
zilizozalishwa katika maeneo yenye ugonjwa.”
Hivyo tunaendelea kusisitiza kuwa
wakulima wawe makini wanapo nunua mbegu kutoka kwa wasambazaji
wasiotambulika na watoe taarifa haraka kwa Bodi wanapoona mbegu hizo
hazioti ili hatua za haraka zichukuliwe za kupeleka mbegu zingine
mbadala ili kuendana na msimu wa kilimo.
Aidha, Bwana Shimbe amewataka
wachambuaji wa pamba ambao ndio wasambazaji wa mbegu kuacha mara moja
kuwasambazia wakulima mbegu ambazo zimetoka kwenye maeneo yaliyobainika
kuwa na ugonjwa na badala yake mbegu za pamba hizo zisindikwe kuzalisha
mafuta ya kula kama walivyokuwa wameelekezwa na Bodi hapo awali.
“ Bodi ilishatoa maelekezo kwa
wachambuaji wote wa pamba kote nchini, kutenga mbegu za pamba za
kupanda msimu huu wa kilimo kutoka maeneo yaliyo salama kwa kuziwekea
lebo ili kuzitofautisha na zile zinazotoka kwenye maeneo yaliyobainika
kuwa na ugonjwa, ambapo zile zinazotoka katika maeneo yenye ugonjwa
zisitumike kama mbegu za kupanda, bali zisindikwe kupata mafuta ya kula
kama sehemu ya kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa, na zile mbegu ambazo
zimetoka kwenye maeneo yasiyo na ugonjwa zisambazwe kwa wakulima kwa
ajili ya kupanda kwenye mashamba yao baada ya kufanyiwa majaribio ya
uotaji (seed germination test) na taasisi inayohusika na udhibiti wa
ubora wa mbegu (TOSCI)”
Aidha, mbegu zinazofaa kutumika
kwa sasa ni UKM08 iliyofanyiwa utafiti na Kituo chetu cha Utafiti cha
Ukiriguru, ambayo ubora wake umethibitishwa na Taasisi ya Kudhibiti
Ubora wa Mbegu (TOSCI) na inauwezo wa kuhimili magonjwa pamoja na
uzalishaji wenye tija zaidi. Mbegu hiyo itakuwa inaiondoa kwenye
uzalishaji ile ya zamani ya UK 91 ambayo imepungua ubora wake. Katika
msimu huu wa kilimo wa 2015/16 Mbegu ya UKM08 itaendelea kuzalishwa kwa
wingi (seed multiplication) katika maeneo salama yasiyo na ugojwa wa
mnyauko fusari katika mkoa wote wa Singida na wilaya ya Nzega na Igunga,
mkoa wa Tabora.
Bwana Shimbe ametoa wito kwa wakulima na wadau wote wa pamba nchini kufuata kanu
ni za kilimo bora cha pamba ikiwa ni pamoja na kutumia mbegu bora za pamba. Aidha, baadhi ya mawakala wa ununuzi wa pamba mbegu na wakulima wenye tabia ya kuchanganya pamba mbegu na maji, mchanga, chumvi na kemikali zingine kama vile “mafuta ya kenge” kwa madai ya kuongeza uzito kwenye pamba yao waachane na tabia hiyo potofu, kwani kwa kufanya hivyo kunachangia kuoza kwa kiini cha mbegu na kuharibu ubora wake na hivyo kusababisha mbegu kutokuota.
ni za kilimo bora cha pamba ikiwa ni pamoja na kutumia mbegu bora za pamba. Aidha, baadhi ya mawakala wa ununuzi wa pamba mbegu na wakulima wenye tabia ya kuchanganya pamba mbegu na maji, mchanga, chumvi na kemikali zingine kama vile “mafuta ya kenge” kwa madai ya kuongeza uzito kwenye pamba yao waachane na tabia hiyo potofu, kwani kwa kufanya hivyo kunachangia kuoza kwa kiini cha mbegu na kuharibu ubora wake na hivyo kusababisha mbegu kutokuota.
Imetolewa:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Tags
HABARI KITAIFA