BANDA MEDIA BLOG

MUSA BILITY NA PLATINI WAONDOLEWA KATIKA MBIO ZA URAIS WA FIFA.

 Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka duniani FIFA limemuondoa katika kinyang’anyiro cha Urais wa FIFA Musa Bility ambaye ni Rais wa chama cha soka cha nchini Liberia.

Bility amekuwa mmoja kati ya watu ambao wameomba kugombea nafasi ya Urais wa FIFA kuchukua nafasi ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter ambaye ameamua kujiuzulu hivi karibuni.
Kamati ya uchaguzi imeamua kumuondoa Musa Bility kwa sababu za Uadilifu baada ya kumchunguza na kujiridhisha kuwa Bility hana sifa ya kubaki kuwa mgombea wa Urais katika uchaguzi mkuu wa FIFA mwezi wa pili tarehe 26 mwaka huu.
Mwingine aliyeondolewa katika kinyang’anyiro hicho ni Rais wa UEFA Michel Platini.
Michel Platini ameondolewa katika kuwania nafasi ya Urais kwa sababu amefungiwa na kamati ya maadili ya FIFA kwa muda wa siku 90 kwa kosa la kuhusika kupokea rushwa toka kwa aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter.
Mpaka sasa hakuna uamuzi uliotolewa juu ya rufaa yake ya kupinga adhabu ya kufungiwa siku 90.
FIFA imetangaza majina matano hii leo ambayo yamebaki katika kinyang’anyiro cha Urais baada ya baadhi ya majina kuchujwa na kamati ya uchaguzi ya FIFA.
Majina yaliyopitishwa ni pamoja na Prince Ali Al Hussein(Jordan), Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa(Bahrain), Jerome Champagne(France), Gianni Infantino(Uswisi) na Tokyo Sexwale (Afrika Kusini)

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG