Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(wa kwanza
kushoto) akiangalia mitambo ya kurushia matangazo ya Shirika la
Utangazaji Tanzania(TBC) wakati alipofanya ziara ya kikazi katika minara
ya shirika hilo leo hii Kisarawe.Profesa Elisante amefanya ziara katika
Taasisi tatu zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Baraza la Sanaa
Tanzabia (BASATA),Tanzania Standard Newspapers(TSN) na Shirika la
Utangazaji Tanzania(TBC) lengo likiwa ni kufahamiana na
wafanyakazi,kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kujua changamoto
zinazowakabili ikiwa ni kutimiza kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya awamu ya
Tano.Anaefuatia ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw.Clement Mshana.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(waliosimama watatu kulia) akiwa katika mojawapo ya studio za kurushia matangazo ya shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wwakati alipotembelea shirika ilo leo kuongea na menejimenti yake pamoja na kuona utendaji wake.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(aliyekaa mwenye miwani) akipata maelekezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mtumishi wa Standard News Papers(TSN) leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi na kuangalia utendaji wa kazi.
Tags
HABARI KITAIFA



