BANDA MEDIA BLOG

MWAMUZI ANUSULIKA KICHAPO CHA MASHABIKI BAADA YA KUKIMBILIA NYUMBA JIRANI


Mchezaji wa Dom City akionyesha uwezo wake wa kumiliki Mpira mbele ya wachezaji wa Fire Stone.
Na John Banda,Dodoma
MWAMUZI Salehe Mang’ola amenusurika kuchezea kichapo kutoka kwa wanaohisiwa kuwa mashabiki wa timu ya Fire Stone kutokana na kutoridhishwa na uamuzi wake katika mchezo wa kombe la Ng’ombe.

Mchezaji wa Dom City ya Nzuguni Bonface Mjerwa akimzidi ujanja Mlinzi wa Fire Stone na kufanikiwa kupata goli kwa kumvisha Kanzu mlinda mlango wa timu hiyo.

Tukio hilo ambalo lilitokea juzi katika uwanja wa Mbuyuni Nzuguni manispaa ya Dodoma wakati timu hiyo ikipambana na Dom City ya nzuguni.

Ilikuwa hivi mara baada ya kupuliza filimbi ya kumaliza pambano hilo wanaohisiwa kuwa ni mashabiki wa Fire Stone walianza kumfukuza mwamuzi huyo ambaye  alitimua mbio hadi katika nyumba zilizopo jirani na uwanja huo.

Mwamuzi huyo mara baada ya kufika katika nyumba hiyo aliingia ndani na kujifungia hali iliyowafanya mashabiki wa timu hiyo kubaki nje wakiwa wanashangaa tu.

Mpira uliopigwa na Mshambulizi Bonface Mjerwa ukiwa umechana nyavu kutokana na shuti kali
Mwamuzi huyo alikaa ndani ya nyumba hiyo kwa zaidi ya dakika 40 akisubiria mashabiki hao waondoke,ambapo mashabiki hao waliondoka huku hasira zao zikiishia kung'oa na kuvunja milingoti ya magoli uwanjani hapo, ndipo alipopata nafasi kuondoka.

Hata hivyo mwamuzi huyo mkongwe alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo aligoma kuongea kwa madai kuwa yeye siyo msemaji wa mchezo huo

Katika mpambano huo wa nusu fainali ya kombe la ng'ombe, Fire Stone ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Dom City iliyojihakikishia kuingia fainali.
mwisho
Mfungaji wa Bao pekee la Dom City akagalagala baada ya kukatwa na mabeki wa timu ya Fire Stone wakati hana Mpira

vita ya soka kwenye mchezo huo
Mwanzo wa kumzonga Mwamuzi
Wachezaji wa timu za Fire Stone na Dom City wakimzonga mwamuzi baada ya wachezaji wa timu hizo kupigana
Mfungaji wa Goli akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya Mwamuzi kudanganywa na wachezaji wa Fire Stone



Mashabiki wanaodhaniwa ni wa timu ya Fire Stone wakimvamia  Mwamuzi Saleh Mang'ola mara baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo huo
Mwamuzi huyo Saleh Mang'ola akaamua kutimua Mbio ili kujiokoa na kipigo toka kwa mashabiki hao mpaka ndani ya nyumba iliyokuwa jirani na Uwanja huo
Mwamuzi akichungulia kwa Mbali kama wabaya wake wameondoka



Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG