Watu wengi wanakimbia baadhi ya
mitaa ya Bujumbura, Burundi, kabla ya muda uliowekwa na serikali wa leo
usiku, ambapo watu wenye silaha wanatakiwa kusalimisha silaha zao.
Umoja wa Mataifa unasema, watu karibu mia mbili wameuwawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili, katika fujo zilizochochewa na tangazo la Rais Pierre Nkurunziza kusema anagombea muhula wa tatu wa uongozi.
Watu zaidi ya laki mbili wamekimbilia nchi za nje.
Katika juma lilopita peke yake, watu 13 wamekufa, hasa kwenye mitaa ambako upinzani una nguvu.
Tags
KIMATAIFA
