BANDA MEDIA BLOG

RAIS WA NIGERIA AMFUKUZA KAZI MKUU WA TAASISI YA KUPAMBANA NA RUSHWA

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amemfukuza kazi mkuu wa taasisi ya kukabiliana na rushwa.

Hakuna sababu zozote zilizotolewa kwa kufukuzwa kazi Bw. Ibrahim Lamorde ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Kupambana na Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha (EFCC).

Agosti mwaka huu Bw. Lamorde alikanusha tuhuma za kuwepo kwa upotevu wa kiasi cha dola bilioni 5, katika tume hiyo.

Rais Muhammadu Buhari alishinda urais mwezi Machi, aliahidi kupambana na rushwa nchini humo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG