Wawezeshaji wa Sheria katika soko la
Mchikichini katika Manispaa ya Ilala, wakiwa na mabango ya mradi wa Mpe
Riziki si Matusi baada ya kuzungumza na waaandishi wa habari Dar es
Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko yaliyopo katika Manispaa hiyo
kuona maendeleo ya vita ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia katika
masoko hayo baada ya Shirika la Equality for Growth linaloendesha mradi
huo kutoa mafunzo kwa Wawezeshaji wa Sheria wanaoshirikiana na
wafanyabiashara katika vita hivyo.
Mwezeshaji wa Sheria, Eva Kakobe akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya ukatili wa jinsia wanavyokabiliana nayo katika soko hilo.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Charles Beatus akichangia kuhusu mwongozo wa kutoa adhabu kwa wanaobainikwa na makosa ya udhalilishaji. Kushoto ni Mtaalamu wa kujitolea wa masuala ya kijinsia kutoka nchini Canada, Ashley Ekelund.
Mwezeshaji wa kisheria katika soko hilo, Domitila Ngwada akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mjumbe wa Bodi ya Sekta ya Kanga na Vitenge katika soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala, Zainabu Namijojo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao wapo katika ziara ya kutembea masoko ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi mradi wa Mpe Riziki si Matusi ulivyowakomboa wanawake katika vita ya kupinga udhalilishaji masokoni unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG). Kulia ni Mwezeshai wa Sheria katika soko hilo, Nechi Omar.
Mfanyabiashara wa vitenge na magauni, Sophia Kizinga akichangia jambo kuhusu kupungua kwa ukatili wa jinsia katika soko hilo.
Mfanyabiashara, Ikram Zubery (katikati), akizungumza na waandishi wa habri kuhusu ukatili wa kijinsia katika soko hilo.

Mama Lishe katika soko hilo, Edwiga Assenga (wa pili kulia), akizungumza na wanahabari waliotembelea soko hilo.
Na Dotto Mwaibale
VYUMBA vilivyokuwa vikitumiwa kwa ajili
ya kupimia nguo kabla ya kuzinunua katika soko la Mchikichini Manispaa
ya Ilala jijini Dar es Salaam vinadaiwa vilikuwa vikitumia kudhalilidha
wateja hasa wanawake.
Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Bodi ya
Sekta ya Kanga na Vitenge katika soko hilo Zainabu Namijojo Dar es
Salaam leo asubuhi, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao
wanafanya ziara ya kutembea masoko ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi
mradi wa Mpe Riziki si Matusi ulivyowakomboa wanawake katika vita ya
kupinga udhalilishaji masokoni unaoendeshwa na Shirika la Equality for
Growth (EfG).
"Katika soko letu tulikuwa na changamoto
kubwa ya udhalilishaji hasa maeneo ya wauza nguo kuu kuu (Mitumba),
kwani walikuwa wakitumia vyumba vidogo vya kujaribishia nguo
kuwadhalilisha wanawake kwa kuwakamata maungoni na kuwawekea kioo chini
ili waweze kuona utupu wao" alisema Namijojo.
Alisema hivi sasa vitendo hivyo vimekoma
baada ya shirika hilo kufanya matamasha na semina mbalimbali na kutoa
mafunzo kwa baadhi yao ambao sasa ni Wawezeshaji wa Sheria katika soko
hilo ambao wamekuwa karibu na wafanyabiashara kufuatilia vitendo vya
udhalilishaji.
Mwezeshaji wa Sheria Domitila Ngwada
alisema vitendo vya ubakaji na matusi ya nguono yalishamiri sana lakini
hivi sasa hali ni nzuri kwani vitendo hivyo vimepungua kwa asilimia 70
ukilisha na hapo awali kabla ya kufikiwa na EfG.
"Tangu kuwepo na wawezeshaji wa Sheria
katika soko letu vijana wengi waliokuwa na vitendo vya kudhalilisha
wanawake wameingiwa na hofu kubwa hasa kupigwa faini zilizowekwa kuanzia
kiwango cha sh.50,000" alisema Ngwada.
Mfanyabiashara katika soko hilo, Ikram
Zuberi alisema jitihada za makusudi zinapaswa kufanyika ili kumaliza
vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika sokjo hilo ingawa kwa kiasi
kikubwa vimepungua kwa msaa wa EfG.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo
Charles Beatus alisema wale wote wanaopatika na makosa ya udhalilishaji
wamekuwa wakiadhibiwa kutokana na mwongozo uliopo na kesi zote zinaanza
kusikilizwa sokoni hapo na ikishindikana upelekwa ngazi nyingine ikiwemo
polisi.
Tags
HABARI KITAIFA