Na Mahmoud Ahmad Arusha
MTU moja amefariki dunia , na vyumba vinne vya madarasa na ofisi mbili za walimu zikiteketea wa moto usiku wa kuamkia leo.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Edward BaleLe, amesema matukio hayo yanatokana na yanzo tofauti .
Amesema mtu mmoja ambae ni
kijana amefariki kwa kuteketea kwa moto alipokuwa amelala kwenye nyumba
ya mzazi wake eneo la Njiro jijini Arusha.
Amesema kulingana na maelezo ya
baba yake na marehemu, ambae ni mhadhiri mstaafu wa chuo ,mtoto wake
alirejea majira ya saa tisa usiku na kuingia ndani ya chumba chake na
baada ya muda mfupi moto ulizuka na kuteketeza nyumba hiyo .
Amesema bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na chanzo cha tukio hilo.
Amesema moto huo unasadikiwa
ulizuka majira ya saa kumi usiku wa kuamkia leo muda mfupi tu baada ya
marehemu kuingia ndani ya nyumba hiyo na kulala na ndipo moto ulipozuka
na kuteketeza nyumba hiyo.
Katika tukio lingine vyumba vinne vya madarasa vimeteketea kwa moto kwenye shule ya msingi ya Daraja mbili ya jijini Arusha.
Kamanda Balele, amesema chanzo
ni hitilafu ya umeme ambayo imesababisha pia ofisi mbili za walimu
kuteketea kwenye tukio hilo na hasara kamili bado haijajulikana.
Wakati huo huo kamanda
wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Aruha, Philemon
Mollel, ambae pia ni mgombea ubunge jimbo la Arusha, amefika kwenye
shule hiyo na kuahidi tofali 2000 za Saruji.
Tags
HABARI KITAIFA
