Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015
na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, wananchi hutumia muda huo kwenda
katika nyumba za ibada ama kusherekea katika maeneo mbalimbali ya
starehe, ambapo uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hupenda kutumia
fursa hiyo kufanya vitendo vinavyohatarisha usalama wa raia mali zao.
Jeshi la Polisi nchini,
limejipanga vizuri katika mikoa yote kwa kushirikiana na vyombo vingine
vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kwamba vitendo vyovyote vya
uhalifu vitakavyojitokeza hususani katika kipindi hiki cha kuelekea
mkesha wa mwaka mpya vinadhibitiwa. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo
yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine
yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa
tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za
haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu
katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara. Simu za polisi
endapo mwananchi atakuwa na taarifa ni 111 au 112.
Pia, Jeshi la Polisi
linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa
makini na kuzingatia sheria za usalama barabar
ani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
ani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Vilevile, wananchi kuacha tabia
ya kuchoma matairi barabani pamoja na kupiga mafataki. Aidha, yeyote
atakayefanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
yake.
Nawatakieni watanzania wote kheri ya mwaka mpya.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Tags
HABARI KITAIFA