BANDA MEDIA BLOG

WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA WAIOMBA SERIKALI KUITUPIA JICHO STAND YA DALADALA SAMUNGE


Mahmoud Ahmad Arusha
…………………………………….
Wakazi wa Arusha na Madereva wa Daladala wameiomba serikali kuikarabati Stand ya daladala iliyopo Samunge kwani ipo kwenye hali mbaya hususani kipindi hiki cha mvua huku pia wakilalamikia msongamano wa magari kwenye lango la kuingilia Stand hiyo hali inayoleleta usumbufu kwa wapita kwa miguu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema kuwa kumekuwa na hali mbaya wakati wa kupanda magari hayo hususani kipindi hichi cha mvua na kuwataka watendaji wa serikali na madiwani kuliangalia hilo ikiwemo kuweka moramu,na vibanda sanjari na kuiboresha Stand hiyo.
Mkazi wa Kata ya Muriet Agnes John alisema kuwa kumekuwa na usumbufu kwa nyakati tofauti kwenye stand hiyo kiasi imekuwa Adha kwa wakazi wanaokwenda kupata huduma kwenye stand hiyo huku akizitaka mamlaka husika kuliangalia suala la uboreshaji wa stand hiyo.
“Jamani hebu tizameni stand hii kwa ukaribu angalia hata sehemu za kupumzikia wanaokuja kupanda basi au wanaosubiria jamaa zao kutoka eneo moja kwenda jingine ni shida hakuna maeneo hayo ni msongamano wa magari bila ya mpangilio haya yanakwenda wapi tunaomba mamlaka ziangilie hili”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji Juma Idd yeye hakuweza kupatikana kwa simu yake ya mkononi na gazeti hili linaendelea kumtafuta ilikulitolea majibu suala hilo ila kwa upande wake Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro alipopigiwa simu na gazeti hili ilikujua baraza lake analoliongoza kama limepanga nini kuhusu Stand hiyo alijibu kuwa yupo kwenye kikao cha elimu na kukata simu yake ya mkononi bila maelezo.
Gazeti hili pia likaongea na mmoja wa madereva wa Dala dala Abdallah Mwarabu alisema kuwa wamekuwa wakifanyakazi kwenye mazingira magumu katika stand hiyo ikiwemo nyakati za jioni kwani ndani ya Stand Taa zilizopo hazitoshelezi na zinawaweka abiria kwenye wakati mgumu hivyo wamekuwa wakipakia nje ya stand hiyo.
Hali ya Stand hiyo ya daladala iliyopo kwenye eneo la Samunge kata ya Levolosi imekuwa mbaya hususa kwenye upitishaji wa maji wakati wa mvua hali inayoleta usumbufu kwa abiria,huku kumekuwa hakuna sehemu ya abiria kupumzikia au kujikinga na mvua wakati wakingojea usafiri kwenye stand hiyo

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG