Ametoa wito huo jana mchana
(Jumamosi, Januari 30, 2016) kwenye uwanja wa Jamhuri wakati akizungumza
na mamia ya viongozi na wananchi mbalimbali walioshiriki mashindano ya
mbio za nusu marathon (km. 21 na km. 5) zilizofanyika mjini Dodoma.
Mashindano hayo yalijulikana kama “HAPA KAZI TU HALF MARATHON”.
“Michezo ni sayansi kwa hiyo
tunahitaji kuwafundisha vijana wetu sayansi ya michezo na kuwapa mbinu
tofauti za kufaulu kwenye mashindano mbalimbali ya kitaifa na
kimataifa,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema wapo Watanzania wachache
ambao wamethubutu kufungua shule za michezo na kuwataja Filbert Bayi
(shule ya Filbert bayi) na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu (shule ya Lord
Baden). “Tumeona matunda ya sports academy hizo kwani zimeibua vijana ambao tayari wameshiriki michuano ya kimataifa,” alisema.
Alisema michezo ina nafasi kubwa
ya kulitangaza Taifa la Tanzania na ndiyo maana Serikali imeamua
kuimarisha sekta ya michezo, utamaduni, sanaa na habari.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu alimpongeza kijana Joseph Stanford ambaye ameamua kutembea kwa
miguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kumuunga mkono Rais Dk. John
Pombbe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi.
Kijana Joseph (19) ambaye
alikuwepo uwanja wa Jamhuri, alisema ametumia siku 13 tangu aanze safari
hiyo ikiwa ni wastani wa km. 80 kwa siku. “Ninatembea kwa saa 12 kwa
siku na ikifika jioni natafuta mahali penye mji na kupumzika,” alisema.
Joseph ambaye amehitimu kidato
cha nne mwaka jana katika shule ya sekondari ya Mtoni iliyoko
Mwanza-Mabatini, amesema hivi sasa anasubiri matokeo ya mitihani yake
lakini ameguswa na utendaji kazi wa Rais Magufuli ndipo akaamua
kuanzisha matembezi hayo ili kumuunga mkono.
Alipoulizwa anafanyaje anapopita
kwenye maeneo ya misitu mikubwa au mapori ya kutisha, Joseph alisema
hajakutana na misitu mikubwa ya kutisha isipokuwa kwenye milima ya
Sekenke na eneo moja kabla ya kuingia mkoa wa Dodoma.
Joseph amesema anatarajia kuanza
safari ya kuelekea Dar es Salaam kesho kutwa (Jumanne, Februari 2, 2016)
kwani anasubiri kukutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Bw. Nape Nnauye hapo kesho.
Tags
MICHEZO KITAIFA