Mbwana Samatta ambaye ni mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika
kwa wachezaji wanaocheza Afrika, leo amefunga mitaa mbalimbali ya jiji
la Dar es Salaam ambapo amezunguka kwenye mitaa ya jiji hilo kuwapelekea
tuzo hiyo wakazi wa Dar es Salaam wakati akielekea kwenye viwanja vya
Escape One ambako inafanyika tafrija ya kumpongeza Samatta.
Safari ya Mbwana Samatta kuelekea kwenye viwanja vya Escape One
ilianzia mtaa wa Samora, Clock Tower, Mnazi mmoja, barabara ya Uhuru,
Kamata hadi Karume.
Kisha msafara huo ukaingia barabara ya Kawawa kuanzia ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kigogo, Magomeni Usalama, Kinondoni hadi
Morocco na kuifuata barabara ya Ally Hassan Mwinyi kupitia Victoria,
Makumbusho, Sayansi, Bamaga hadi Mwenge.
Msafara huo ukazungukia Kawe, Lugalo, Mlalakuwa, na kumalizikia
Escape One ambapo watu mbalimbali pamoja na mashabiki watapata fursa ya
kupiga picha na shujaa huyo wa Tanzania.
Samatta pamoja na viongozi wa Wizara yenye dhamana ya michezo wakiwa kwenye picha ya pamojaSamatta akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape NnauyeMh. Nape Nnauye akiwa mwenye furaha muda woteShabiki naye akaamua kutoa zawadi yake ya puto kwa Samatta yote ikiwa ni katika ku-show loveSamatta akicheza na puto ambalo alipewa na moja ya mamia ya mshabikiAsikwambie
mtu, bodaboda walisimamisha huduma ya usafiri wakahamia kwenye msafara
wa Samatta na hapa wao ndiyo wanaongoza safari wakiwa mbele kabisaIlipobidi kuwapa tano washkaji jamaa hakuacha kufanya hivyo na hii inaashisi ni kiasi gani alivyokuwa mtu wa watuSamatta akipunga mkono kuwasalimia mashabiki waliojitokeza kumlaki alipopita mitaaniSamatta akiwa ameishikilia tuzo yake vizuri kutoa nafasi kwa waandishi kupiga picha za kumbukumbu
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye Sambamba na
Shujaa wa kweli wakiwa kwenye gari la kweli wakipita mitaani kuwaonesha
watanzania tuzo aliyoshinda Samatta
Shaffih
Dauda akisalimiana na makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange
‘Kaburu’ kwenye sherehe za kupongeza Samatta kwenye viwanja vya Escape
OneSamatta na Kaburu katika picha ya pamoja wakiwa wameshika tuzoSamatta
akisalimiana na makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’
aliyesafiri kutoka Zanzibar yanakofanyika mashindano ya Mapinzuzi ambapo
Simba imeingia nusu fainali akarejea Dar kumpongeza Samatta ambaye
alijiunga na TP Mazembe akitokea Simba SCViongozi
wa Serikali wakifurahi pamoja na Samatta lakini akiwepo pia mchezaji
mwenzake wa klabu ya TP Mazembe Thomas Ulimwengu pamoja na katibu mkuu
wa TFF Celestne MwesigwaWaziri
wa wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye pamoja na
Mh. January Makamba Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi,
Muungano na MazingiraSamatta pamoja na Dauda wakiteta jambo
Mashabiki waliojitokeza kwenye party ya kumpongeza Samatta viwanja vya Escape One wakimlaki shujaa wao Mbwana Samatta