BANDA MEDIA BLOG

MWANAMKE ALIYEOLEWA NA WANAUME WAWILI AFANIKIWA KUVUNJA NDOA MOJA

Matumaini ya mwanamke wa Mombasa Kenya aliyeolewa na wanaume wawili ya kutaka kutengana na mume wake wa kwanza ambaye mapenzi yamechuja, yamefanikiwa baada ya mahakama kuridhia kuvunja ndoa yake hiyo.

Hata hivyo, hukumu ya Mahakama ya Kadhi imemuagiza mwanamke huyo Rehema Dzuya kurejesha mahari ya samani za ndani zenye thamani ya shilingi 40,000 za Kenya alizotoa mumewe kama mahari.

Hata hivyo mume wa Rehema, Salim Twota amepinga maamuzi hayo ya Mahakama ya Kadhi, kwa madai kuwa yamempendelea mkewe, na kukesma atakata rufaa katika Mahakama Kuu kwa kuwa bado anampenda mkewe.

Kadhi Mkuu wa Mombasa Abdulhamin Athman amevunja ndoa hiyo kwa kusema ni vigumu sana kwa Rehema na mumewe Salim kuishi pamoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG