Waziri wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba akimsikiliza mmoja wa wakulima wa vyama binafsi.
Waziri wa Kilimo Mh Mwigulu Nchemba ( kulia ) akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mh Amina Masenza baada ya kuwasili mkoani Iringa. Pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh Richard Kasesela.Waziri wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa.
Wakulima
wamelalamika sana uchelewashwaji wa pembejeo, bei duni ikiwemo madaraja
mengi ya mfano kuna madaraja zaidi 72 ya grade za tumbaku kitu ambach
wakulima wamesema inawaumiza sana kwenye bei.
Pia wakulima wamelalamika ubadhirifu wa chama cha mtandao (Union) kiitwacho ITCOJE.
Katika
ziara hiyo Mh Waziri aliambatana na Mrajisi wa vyama vya ushirika Dr
Rutabanzibwa na Mkurugenzi wa bodi ya Tumbaku Bwana Mushi. Mh Waziri
ameagiza matatizo mengi yawe yametattuliwa kabla kikao cha bunge
hakijaanza.
Mh Mwigulu aliwasili kwanza ofisi ya Mkuu wa mkoa na kupokewa na Mkuu wa Mkoa Mh Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela. Mh Masenza alimpa taarifa fupi ya hali ya Kilimo katika mkoa wa IRINGA.

Mkutano ukiendelea
Tags
HABARI KITAIFA