BANDA MEDIA BLOG

SAMATTA ATIMKIA NIGERIA KUTAFUTA HESHIMA YA TANZANIA

Mbwana Samatta (katikati) akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine (kulia) pamoja na mwandishi na mchambuzi wa michezo wa Clouds Media Group na shaffihdauda.co.tz
Mbwana Samatta (katikati) akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine (kulia) pamoja na mwandishi na mchambuzi wa michezo wa Clouds Media Group na shaffihdauda.co.tz
Mambo tayari yameshaiva, mshambuliaji nyota wa Tanzania Mbwana Samatta ameiacha ardhi ya Bongo  usiku wa kuamkia leo (January 6, 2015) na kupaa kuelekea jijini Abuja, Nigeria kwenye sherehe za ugawaji wa tuzo za mchezaji bora Afrika kwa mwaka 2025 (Glo-CAF Awards) ambazo zitakabidhiwa kwa washindi January 7, 2026.
Samatta ameingia fainali ya kinyang’anyiro cha tuzo ya mchezaji bora Afrika 2015 anayecheza soka ndani ya Afrika baada ya kupata mafanikio makubwa na klabu yake ya TP Mazembe kwa mwaka 2015.
Mbwana Samatta akifanyiwa mahojiano na kituo cha television cha Azam TV muda mfupi kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam kuelekea Abuja
Mbwana Samatta akifanyiwa mahojiano na kituo cha television cha Azam TV muda mfupi kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam kuelekea Abuja
Samatta ameisaidia Mazembe kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika lakini pia akiibuka mfungaji bora wa mashindano kwa kufikisha jumla ya magoli saba (7) sawa na mshambuliaji Bakri Almadina anayekipiga kwenye klabu ya Al-Marreikh Omdurman ya Sudan.
Samatta ameingia fainali kuwania uzo hiyo pamoja na mchezaji mwenzake wa timu moja Robert Kidiaba ambao wote kwa pamoja waliiwezesha TP Mazembe kunyakua ubingwa wa Afrika kwa ngazi ya vilabu lakini pia kwenye orodha hiyo ya wachezaji watatu yupo mshambuliaji wa kimataifa wa Algeria Baghdad Bounedjah anayecheza klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia ambaye pia ameisadia klabu yake kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Mwandishi na mchambuzi wa michezo Shaffih Dauda akihojiwa na kituo cha Azam TV muda mfupi kabla ya kuondoka uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam kuelekea Abuja-Nigeria kushuhudia ugawaji wa uzo za wanamichezo waliofanya vizuri mwaka 2015
Mwandishi na mchambuzi wa michezo Shaffih Dauda akihojiwa na kituo cha Azam TV muda mfupi kabla ya kuondoka uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam kuelekea Abuja-Nigeria kushuhudia ugawaji wa tuzo za wanamichezo waliofanya vizuri mwaka 2015
Endapo Samatta atafanikiwa kutwaa tuzo hiyo ataingia kwenye kitabu cha rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kutwaa tuzo ya mcheaji bora wa Afrika ukiachana na rekodi waliyoweka yeye na Ulimwengu ya kuwa watanzania wa kwanza kutwaa ndoo ya klabu bingwa Afrika.
Mbwana Samatta (katikati) akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine (kulia) pamoja na Shaffih Dauda (kushoto) mwadishi mwandamizi wa Clouds Media Group na shaffhdauda.co.tz
Siku chache kabla ya Samatta kuelekea nchini Nigeria, alimtembelea Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh. Nape Nnauye ambaye kwa niaba ya serikali, Nnauye alimpa Samatta Baraka zote kuelekea tuzo hizo huku akimtabilia Samatta kuibuka mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG