PICHA: ANGALIA ‘TIMBWILI’ LA YANGA VS AZAM KAMA SOKA LA KITAA VILE
byJohn Banda-
0
Wachezaji wa Azam na Yanga wakiwa katika zogo lililosababishwa na Ngoma ns Pascal Wawa
Jana usiku lilipigwa pambano kati ya Yanga SC dhidi ya Azam FC mchezo
wa Mapinduzi Cup ambao ulikuwa umejaa ubabe mwingi mithili ya pambano
la Francis Cheka vs Thomas Mashali. Wawa (kulia) akijibizana mbovu na Donald Ngoma aliyeshikiliwa na golikipa wa Azam Aishi Manula
Kutokana na nidhamu mbovu iliyooneshwa na wachezaji wa timu zote
mbili pamoja na viongozi wao wakiwemo makocha, mwamuzi wa mchezo huo
alilazimika kutoa kadi nyingi za njano pamoja na kadi moja nyekundu
ambayo ilikwenda kwa John Bocco. Aishi Manula akijitahidi kumshawishi Donald Ngoma apunguze vurugu
Kiukweli mashabiki wa soka wa Zanzibar walijitahidi kujitokeza
uwanjani kushuhudia mchezo huo lakini hakukuwa na jipya zaidi ya
wacheaji kupigana viatu hadi ngumi pia. Mashabiki walifurika uwanjani hadi wakakaa chini kufuatia kukosa nafasi
Mechi hiyo ilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1
Azam na Yanga zinakimbizana kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,
Azam wako kileleni wakati Yanga wao wako nafasi ya pili kwa tofauti ya
pointi mbili. Mashabiki wa Yanga wakiisapport timu yao
Matokeo ya jana yanaiweka pabaya Azam FC ambayo imetoka sare kwenye
michezo miwili hivyo inapointi mbili wakati Yanga na Mtibwa zikiwa na
pointi nne kila moja lakini zikitofautishwa kwa tofauti ya wastani wa
magoli ya kufungwa na kufunga. Mechi ilianza vizuri lakini kadiri muda ulivyokwenda ndivyo mambo yalivyochachaKikosi cha Azam FC kilichoanzishwa na koch Stewart Hall dhidi ya YangaWatoto nwa Jangwani walianza kwenye mchezo dhidi ya Azam FC