Kichuya ameiambia shaffihdauda.co.tz kuwa, yeye binafsi amesikitishwa na taarifa hiyo kwasababu yeye (mwamuzi) pia ni binadamu na anaweza kukosea kama binadamu wengine lakini akaongeza kuwa u-referee ni kazi yake ambayo inampatia kipato na kumfungia ni kumzua asipate pesa ambayo alikuwa anapata kutoka kwenye mashindano hayo.
“Unajua yule pia ni binadamu, huenda ilikuwa ni kosa la kibinadamu kwahiyo siwezi kumlaumu sana kwasababu labda hata angekuwa mwamuzi mwingine angekosea pia”, amesema Kichuya ambaye goli lake lililokataliwa ndiyo limemwondoa mwamuzi huyo kwenye mashindano.
“Lakini kibaya na kinachonisikitisha ni kwamba, ureferee ni kazi yake inayomuingizia kipato hivyo kumfungia inaamaana kwamba hapati tena miambili-miambili alizokuwa anazipata kutokana na mashindano haya”.
Lakini Kichuya amewaonya waamuzi kuwa makini muda wote wa mchezo ili kuzuia makosa ambayo yanaweza kuepukika ili kukwepa lawama pamoja na kufungiwa ili kuufanya mchezo wa soka kuwa mchezo wa kiungana.
Tags
MICHEZO KITAIFA