BANDA MEDIA BLOG

VIKOSI VYA ULINZI VYA BURUNDI VYADAIWA KUBAKA WANAWAKE

Umoja wa Mataifa umesema kuwa kunaushahidi kwamba vikosi vya ulinzi vya Burundi vimewabaka wanawake wakati vikifanya msako kwenye nyumba za wanaume wanashukiwa kuwa ni viongozi wa upinzani.

Umoja wa Mataifa umesema umeandikisha maelezo ya matukio 13 ya ubakaji ambapo vikosi vya ulinzi vya Burundi viliwatenganisha wanawake na kuwabaka.

Vikosi hivyo vya ulinzi pia vimedaiwa kuteka, kutesa na kuwauwa makumi ya wanaume taarifa ya umoja huo imesema.


Wakati huo huo mahakama imewahukumu majenerali wanne kifungo cha maisha jela kwa kujaribu kumpindua rais Pierre Nkurunziza mwezi Mei mwaka jana.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG