![]() |
| Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi. |
![]() |
| Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu Majaliwa. |
![]() |
| Waziri Mkuu akislimiana na Mstahiki meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya . |
![]() |
| Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara ya kushtukiza. |
![]() |
| Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia pcha za mionzi (X Ray) katika hosspitali ya rufaa ya Mawenzi. |
![]() |
| Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo wagonjwa wanahudumiwa. |
![]() |
| Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Mtumwa mwako. |
![]() |
| Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa. |
![]() |
| Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika mkutano huo. |
![]() |
| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia walipokutana Ikulu ndogo mjini Moshi. |
![]() |
| Baadhi ya Viongozi walifika Ikulu ndogo mjini Moshi kwa ajili ya kumsikiliza ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini. |
……………………………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewasili mkoani Kilimanjaro na kufanya ziara kushtukiza kwenye
hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali ya mkoa huo.
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye mara
baada ya kuwasili Ikulu ndogo ya Moshi mjini jana jioni (Jumamosi,
Januari 30, 2016) alipangiwa kupokea taarifa ya mkoa huo, alimweleza
Mkuu wa mkoa huo kwamba anataka kufanya ziara katika hospitali hiyo na
kuwaomba radhi watendaji waliokuwa wanasubiri taarifa ya mkoa
iwasilishwe.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu ameamua
kufanya ziara katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali
yetu ya mkoa na atakuja kupokea taarifa ya mkoa wetu tukishatoka huko,”
alisema Mkuu wa mkoa huo, Bw. Amos Makalla.
Mara baada ya kuwasili
hospitalini, Waziri Mkuu alielekeza apelekwe kwenye chumba cha upasuaji
(theatre) huku akimuuliza maswali kadhaa Mganga Mfawidhi wa hospitali
hiyo, Dk. Bingileki Lwezaula.
Katika chumba cha upasuaji
ilibainika kuwa kuna vyumba vitatu vya kufanyia upasuaji lakini
kinachotumika ni kimoja tu kwa sababu vingine havina dawa za kulaza
wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji (anesthesia) licha ya kuwa jengo la
upasuaji lina mwaka sasa tangu lilipozinduliwa Februari, 2015 na Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete.
Akiwa katika wodi ya utabibu ya
wanawake, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa juu ya
kukosekana kwa dawa hospitalini hapo. Afisa Muuguzi wa wodi hiyo, Bi.
Anjela Mwakalile alisema wametuma maombi ya kupatiwa dawa kutoka MSD
lakini bado hazijafika.
Hali hiyo ilijitokeza pia kwenye
wodi ya watoto. Akizungumza na wazazi wa watoto aliowakuta wamelazwa,
mama mmoja alimweleza Waziri Mkuu kwamba sera ya Taifa inasema watoto
wachanga hadi walio na miaka mitano wanapaswa kupata matibabu bure,
lakini wao hapo hospitalini wanalazimika kununua dawa.
Waziri Mkuu alimtaka Mganga Mkuu
wa Mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako kubadili haraka mfumo wa uagizaji wa dawa
baada ya kupokea maelezo ya Dk. Lwezaula kwamba wametuma maombi MSD
tangu miezi miwili iliyopita lakini hadi sasa hawajaletewa dawa
walizoomba.
“RMO ni kwa nini hamuwezi kuagiza
dawa nyingi (bulk) kwa magonjwa ambayo mnajua yanajirudia mara kwa mara
ili wagonjwa weu wasipate usumbufu? Hii ni hospitali ya mkoa na mgao wa
dawa unaopaswa kuja hapa ni wa level ya mkoa? Haiwezekani mnafanya
hivyo ili wagonjwa wajinunulie dawa kutoka kwenye maduka yenu?,” alihoji
Waziri Mkuu.
“Hii hospitali ni kubwa kuliko
idadi ya wagonjwa wanaofika kutibiwa hapa na hii ni kwa sababu wengi wao
wanaishia kwenye hospitali za wilaya. Kwa hiyo mlipaswa kuwa na dawa za
kutosha. Wodini nimekuta wagonjwa wachache katika wodi nilizopita, ina
maana mna ahueni hapa… mnao madaktari wa kutosha, wataalamu 12, lakini
ni kwa nini hakuna dawa za kutosha?” alihoji.
Wakati akitoka wodi ya watoto,
kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Hussein ambaye
anauguza mgonjwa wake hospitalini hapo alimweleza Waziri Mkuu kwamba
dawa pekee wanayopatiwa kwenye hospitali hiyo ni paracetamol tu.
“Hapa dawa ya bure pekee unayopata ni paracetamol tu. Dawa nyingine zote unaandikiwa ukanunue maduka ya nje. Na ukizipata ni kati ya sh. 60,000/- hadi 70,000/- kwa mkupuo.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Severine
Kahitwa apeleke maombi ya kupatiwa mafundi wa mashine za xray haraka iwezekanavyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo
baada ya kukuta mashine kubwa kwenye chumba cha mionzi cha hospitali
haifanyi kazi na inayofanya kazi ni ndogo haiwezi kufanya baadhi ya
vipimo.
Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa kitengo cha Radiolojia, Dk. Ephraim Minja alisema: “Tuliambiwa spare parts zimekwama bandarini, na vifaa hivyo vikipatikana vitaweza kutatua tatizo lililopo.”
Alipoulizwa na Waziri Mkuu kabla
ya mashine ya kuharibika alikuwa akihudumia wagonjwa wangapi, Dk. Minja
alisema kwa wastani alikuwa akihudumia wagonjwa 60 hadi 70. “RAS
fuatilia mafundi kwa Katibu Wizara ya Afya. Hii ni hospitali kubwa tena
ya Serikali kwa hiyo haiwezekani wagonjwa waje hapa na kuambiwa waende
kupata vipimo mtaani,” alisema.
Tags
AFYA




















