Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akishiriki katika kazi ya kujenga msingi wa chumba
cha maabara katika shule ya sekondari kata ya Unyanga Singida ikiwa ni
shuguhuli za maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM
yanayotarajiwa kufanyika mjini Singida Jumamosi Februari 6 mwaka huu
kwenye uwanja wa michezo wa Namfua mkoani humo, Kauli mbiu ya
maadhimisho ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi” (PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-SINGIDA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akishirikiana na mafundi katika ujenzi wa msingi
chumba cha maabara sekondari ya kata ya Unyanga Singida tayari kwa
maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa
kufanyika mjini Singida Jumamosi Februari 6 mwaka huu kwenye uwanja wa
michezo wa Namfua mkoani humo.
Baadhi ya wananchi wakiendelea na akzi ya kuchanganya mchanga na sementi kwa ajili ya ujenzi wa maabara hiyo.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na kazi yao katika ujenzi huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akisshiriki katika kazi ya kupalilia shamba kwa
kutumia mifugo yaani Ng’ombe na jembe la Plau katika shamba la mtama la
mkulima Elisha Abdalla lenye ukubwa wa ekari moja na nusu katika kata
ya Mtamaa wilayani Singida Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi”
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi katika shamba hilo.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi”
Mkulima Bw . Elisha Abdalla akimuelezea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jinsi anavyolima shamba lake kisasa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi mara baada ya kushiriki kazi
ya kupalilia shamba la mtama la Bw. Elisha Abdalla wa kata ya Mtamaa
wilayani Singida.
Baadhi ya wajasiriamali wa wilaya
ya Singida wanaojishghulisha na biashara ya Mama Ntilie, Bodaboda na
matunda wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika
mkutano uliofanyika kwenye ofisi ya CCM mkoa wa Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akizungumza na wajasirialmali wa mjini Singida wakati
alipokutana nao kwenye ofisi ya CCM mkoa wa Singida na kusikiliza
matatizo yao ili kuyapatia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akimsikiliza Afisa biashara wa Manispaa ya
SingidaBwErick Sinkwembe wakati alipokutana na wajasiriamali kwenye
ofisi ya CCM mkoa wa Singida na kusikiliza matatizo yao ili kuyapatia
ufumbuzi.
Tags
SIASA