Gari hilo la Suzuki Vitara linavyoonekana kwa nyuma.
Gari hilo aina ya Suzuki Grand Vitara linavyoonekana ubavuni.
Moja
ya Suzuki magari ya CFAO yaliyopo kwenye maonyesho ya bidhaa mpya
walizonazo katika jengo la PSPF Golden Jubilee Tower lililopo Posta
jijini Dar es Salaam.
Suzuki hiyo inavyookena upande wa nyuma.
Gari ndogo Suzuki OMNI inavyookena kwa mbele.
upande
wa ndani unaogawa gari hilo la Suzuki ambao unaonesha upande wa dereva
na upande ambao mtu anaweza kutumia kwa kuweka mizigo na mambo mengine.
upande wa nyuma wa ndaniu wa gari hilo aina Suzuki OMNI.
…………………………………………………………………………
Kampuni ya uuzaji magari ya CFAO
imefanya onyesho la kuonyesha bidhaa mpya walizonazo katika jengo la
PSPF Golden Jubilee Tower lililopo Posta jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Modewji Blog,
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Sheikha Said amesema sababu ya kampuni
hiyo kufanya onyesho katika jengo hilo ni kuwaonyesha wateja wa kampuni
hiyo bidhaa mpya walizonazo katika sehemu zao wanazouzia magari
(showroom).
Amebainisha kuwa, mbali na
kuwaonyesha wateja lakini pia kuwaonyesha wafanyakazi na wananchi
mbalimbali ambao walikuwa hawajui bidhaa zinazopatikana CFAO Motors au
kwa wengine kuwa na shughuli nyingi hivyo kushindwa kufika katika
‘showroom’ zao na kupitia onyesho hilo wataweza kupata magari katika
maeneo yao ya kazi.
“Tupo hapa kwa hili kuwasogezea
huduma watu wa aina mbalimbali na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali
waone bidhaa tulizonazo,” alisema Bi. Said.
Nae Afisa Mauzo wa Suzuki, David
Kritsos alisema kupitia onyesho hilo wananchi na wafanyakazi wa ofisi
mbalimbali wanaweza kununua magari wanayopendelea na wanaweza kusaidiwa
na CFAO Motors kupata mkopo benki ili waweze kupata fedha za kununua
magari hayo na kulipa mkopo taratibu.
Alisema CFAO ndiyo kampuni pekee
nchini yenye nafasi ya kusambaza bidhaa za Suzuki na magari yote
wanayoyauza bado ni mapya yakiwa bado hayajatumika kabisa.
Showroom hiyo itaendelea hadi hapo 4 Februari.
Tags
BIASHARA