BANDA MEDIA BLOG

DK. SALIM KUZINDUA KITUO CHA UTAFITI NA MAFUNZO YA UYOGA CHA CHUO KIKUU CHA KAIRUKI

 Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert Kairuki yatakayofanyika kuanzia Februari 4. Kushoto ni Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni.
 Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN), Dk. Muganyizi Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert
Kairuki yatakayofanyika Februari 4. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu
ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni na Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni. 
…………………………………………………………………………………..
Katika  kuadhimisha miaka 17 ya kumbukuzi ya mwaasisi wa chuo kikuu  cha  kumbukumbu ya Hubert kairuki kuanzia tarehe  4 hadi  6 Feb ambayo  itakuwa ni siku  ya kilele.Mh Dr Salmin
Ahmed Salim  ambaye  pia ndio mkuu wa chuo hicho atazindua jengo la
utafiti  na  mafunzo ya Uyoga  lililopo huko  Boko katika eneo la chuo hicho.

Sambamba na uzinduzi huo  pia shughuli  nyingine katika  kumbukizo hizo  itakuwa ni pamoja na muhadhara kuhusu Uyoga utakaotolewa na
Profesa  Keto  Mshigeni  ambaye ndiye  makamu mkuu  wa chuo hicho  na mwanasayansi aliyebobea katika  tafiti  za uyoga.

Pia  hospital  ya Kairuki it ataendesha zoezi maalum la upimaji na matibabu ya
macho  bila  ya malipo kwa siku  mbili  mfululizo.

Pia patakuwepo matembezi ya hiara kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo  ya
saratani ya kizazi.

Aidha  wanafunzi wa zamani wa chuo  hicho waliopo  Mwanza  na mikoa ya kanda ya ziwa wataadhimisha
kumbukizo hizo  kwa  kufanya  zoezi la kupima afya
bure  kwa wakazi  wa huko.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG