Na Nyakongo Manyama -MAELEZO-Dar Es SalaaM
Halmashauri ya Wilaya ya Butiama
Mkoani Mara imesema imepata ufumbuzi wa changamoto ya wanafunzi
wa darasa la kwanza na awali Shule ya Msingi Mwibagi wilayani waliokosa
mahali pa kusomea kwa kuwagawa wanafunzi hao kwa awamu mbili.
Hayo yamebainishwa leo (Alhamisi
04, Februari 2016), Afisa Elimu wa Wilaya hiyo, Hans Mgaya, wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hii, ambapo alikiri kuwepo kwa
changamoto ya uhaba wa madarasa shuleni kutokana na ongezeko la
wanafanuzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza mwaka huu, ambapo
hata hivyo tayari wameshachukua hatua mbalimbali za kukabiliana na
tatizo hilo.
Aidha, Mgaya amesema kuwa
jitihada za muda mfupi walizozifanya ni kuwagawa wanafunzi hao katika
mikondo miwili ili waweze kubadilishana madarasa , mkondo mmoja utaingia
asubuhi na mkondo mwingine mchana.
Kwa mujibu wa Mgaya alisema
jitihada za muda mrefu ni kujenga shule nyingine mpya ili kusaidia
kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja, ujenzi wa shule hiyo
ulishaanza kabla ya tamko la elimu bure na tupo katika hatua ya awali
ya ujenzi wa msingi wa madarasa hayo alisema Mgaya.
“wanafunzi walioandikishwa
kujiunga na shule ya msingi kwa mwaka huu 2016 imeongezeka kwa kiasi
kikubwa hivyo kusababisha idadi ya wanafunzi kuwa kubwa” alisema Mgaya.
Idadi ya wanafunzi wa darasa la
awali na la kwanza walioandikishwa kwa mwaka 2016 katika shule ya msingi
Butiama kuanza masomo, ambapo hata hivyo zaidi ya wanafunzi 240 wa
shule hiyo wanasomea katika chumba kimoja.
Tags
ELIMU