BANDA MEDIA BLOG

HUMPHREY POLEPOLE:ASEMA DC KASESELA NI HAZINA YA TAIFA


Bw Polepole akimpongeza mkuu  wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela wakati wa kongamano la shirikisho la vyuo vya elimu ya  juu la  wana CCM mkoa wa Iringa jana

.Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw  Richard Kasesela akiwa amembeba mmoja
kati ya watoto wakazi wa  kijiji  cha Mboliboli tarafa ya Pawaga wilaya
ya Iringa ambao wamekumbwa na mafuriko ambayo maji yake yana vimelea
vya ugonjwa wa kipindupindu  kwa  zaidi ya  siku nne sasa baadhi  yao
bado wanaishi juu ya vichuguu
Mkuu  wa  wilaya ya Iringa akizungunza na wananchi  waliookolewa katika mafuriko Pawaga

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw Richard Kasesela akizungumza na  wanafuzi  wa vyuo vikuu mkoa  wa Iringa  wakati wa kongamano la jana kushoto ni Bw Polepole na kulia na kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Bw  salim Asas  na katibu  wa shirikisho hilo Bi mariam Fundi 
………………………………………………………………………………………………………………
Na MatukiodaimaBlog
 
Huku akidai kuwa kazi  inayoendelea kufanywa na rais Dr Magufuli ya
kutumbua majipu wapo ambao wanaumizwa zaidi kutokana na kupoteza imani
ya kuendelea kuishi maisha ya kula bata kila  uchwao.
 
Bw Polepole ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano la miaka 39 ya
kuzaliwa kwa CCM na siku  100 za Rais Dr Magufuli lililoandaliwa na
shirikisho  la vyuo  vya  elimu ya  juu la chama cha Mapinduzi (CCM)
mkoani  Iringa lililofanyika  jana  mjini hapa alisema  kuwa amepata
kushuhudia kupitia vyombo vya habari mbali mbali jinsi ambavyo mkuu
huyo wa wilaya ya  Iringa Bw Kasesela anavyojitolea  kuokoa maisha ya
wananchi wake jambo ambalo kwa viongozi  wengine ni vigumu kufanya
hivyo.
 
Alisema kuwa kati ya wakuu  wa  wilaya ambao wamekuwa wakiitambua kazi yao kwa
wananchi na wananchi wakiona bila tatizo kazi inayofanywa na kiongozi
wao ni pamoja na mkuu  huyo  wa wilaya ya Iringa ambae ushujaa na
uzalendo  wake kwa  wananchi  wake ni mkubwa na mfano  wa  kuigwa na
viongozi wengine katika kuwatumikia  wananchi.
Tanzania  ya Rais Dr Magufuli itapiga hatua  kubwa  zaidi ya leo
tunapotathimini siku 100  za utawala  wake  iwapo watendaji  wote
watatambua wajibu  wao kwa  wananchi wao badala ya kutangulia maslahi
yao kwa  taifa yao….nimependezwa  sana na moyo  wa  kujitolea kwa
ajili ya wananchi ambao mkuu huyu wa wilaya kakangu Richard Kasesela
anaonyesha ni mmoja kati ya wakuu  wa wilaya ambao wanafanya kazi kwa
moyo …..nimeona katika mitandao ya  kijamii mkuu  huyu wa  wilaya
akiogelea katika maji kuokoa maisha ya wananchi  wake ambao wamekubwa na
mafuriko tena maji yenye vimelea vya  kipindupindu ….ni nani angeweza
kuhatarisha maisha yake  hivi zaidi ya kutuma waliopo chini yake
kufanya kazi kwa niaba  yake” alihoji Bw polepole 
 
Huku akimtaka  mkuu   huyo  wa  wilaya  kuzidi  kutumika vema kwa ajili ya
wananchi  wake na  kuomba iwapo inawezekana Rais Dr Magufuli kwenye
utumbuaji  wake  wa majipu kwa wakuu  wa  wilaya na mikoa kuangalia
wakuu  wa wilaya wasio tambua wajibu  wao ambao wapo kwa ajili ya faida
yao na  kuwaacha ama  kuwapandisha vyeo  zaidi   wale ambao wamekuwa
wakifanya  vizuri .

Simpigii debe Kasesela  ila naongea ukweli ulio  wazi kwa  kila mmoja
wenu hasa  watu  wa Iringa ambao mmekuwa  nae ….binafsi nimevutiwa na
utendaji  wake mzuri nampongeza  sana”
 
Hata  hivyo Bw Polepole  alisema  kuwa kazi  inayofanywa na Rais Dr Magufuli
ya kutumbua majipu ni kazi ya nzuri  kwa  watanzania  swapenda uzalendo
ila wapo  wanaoumia kwa ndugu  zao ama wenyewe kutokuwa na uhakika  wa
kuendelea  kufanya anasa za matumizi ya pesa ama kupata mkate wa  kila
siku.
Hii  ni kazi nzuri sana na inapaswa  kuendelea  kwa nguvu zote …ila
tuwe  wakweli hapa wengi  tunashangilia  kuona majipu ambayo si ndugu
yanatumbuliwa hivi inakuwaje kama zamu ya  kutumbua jipu ingekuhusu wewe
ama mzazi  wako …..bila shaka ungeona  zoezi hili ni baya  zaidi
lakini kwa  ajili ya  kuifanya Tanzania kuwa ya  wote lazima  tuwe
wapole tuache kila jipu  litumbuliwe  kwa afya yako “
Aidha  alisema utendaji mzuri  wa Dr Magufuli na  serikali yake ya CCM
umepelekea wapinzani nchini  kukosa hoja ya kuzungumza na kuendelea
kuokoteza maneno ya  kuongea ili mradi  waonekane wameongea jambo lakini
kimoyo  moyo  wanapongeza kazi nzuri ya serikali ya CCM chini ya rais
Dr Magufuli.
Pia alipongeza imani  kubwa ya  wanachama wa chama  cha Demokrasia na
maendeleo (Chadema) kutoka  vyuo vikuu vya  Iringa ambao wamehama
vyama  hivyo na  kujiunga na CCM baada ya kupendezwa  na utendaji mzuri
wa Rais Dr Magufuli katika  kutekeleza Ilani ya  CCM na  kuwataka
wengine kuzidi kurudi CCM kwani wapende  wasipende kasi ya rais Dr
Magufuli ni  kubwa tofauti na  walivyotegemea.
Kwa  upande  wake  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw kasesela pamoja na
kumpongeza Bw polepole kwa kuendelea kuelimisha  umma kupitia vyombo
mbali mbali  vya habari  juu sera  nzuri  za CCM na  kutambua kazi
anayoifanya yeye kama mkuu  wa wilaya ,bado  alitaka wasomi nchini
kutokubali kupandikizwa siasa chafu  za kulalamika na kutuhumu kila
uchwao na badala  yake  wao kuwa msaada kwa umma .
 
Alisema  wapo baadhi ya  wana siasa  wanatumia wasomi kuhadaha  umma kwa faida
yao badala ya  kuelimisha  umma kwa  kueleza ukweli nini CCM imefanya
kwa  miaka yake 39 
 
“wapo  baadhi ya wanasiasa wao kazi kwao ni kusema ovyo ovyo  serikali
ya CCM na  wengine wapo hadi Iringa ambao  wao bila kutukana ama
kuisema vibaya  serikali ya CCM kwao  siku haijapita …. binafsi
sitanyamaza kuona mwana siasa ama mtu  yeyote akimsema ovyoovyo  Rais
wangu Dr John Pombe Magufuli kama akiongea mbele  yangu ngumi moja
mbili nitampa na akiongeza mbali ya mimi kama katika vyombo  vya habari
nitamjibu haraka…..siwezi hata  siku moja  kuvumilia mtu msema ovyo
heri hata  huu ukuu  wa wilaya  nipoteze kwa kuitetea serikali yangu  ya
CCM”

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG