Mradi wa Maji unaohudumia Kijiji cha Peruhanda, Wilaya ya Njombe.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge akikagua chanzo cha maji cha Nyenga kinachohudumia
Mji wa Njombe, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi
wa Mazingira Njombe (NJUWASA), Inj. Daudi Majani
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ubampa, Kata ya
Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Abbas Kandoro
(kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Gulamhussein Kifu.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge mara baada kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji
wa Kijiji cha Ubampa, Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali na Mbunge wa
Jimbo la Mbarali, Haroon Pir Mohamed.
……………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge amezionya Halmashauri za Wilaya za Njombe na Mbarali
kuhakikisha fedha za miradi ya maji zinazotolewa na Serikali,
zinasimamiwa vizuri na kutekeleza miradi ya maji na si vinginevyo.
Mhe. Lwenge alisema hayo mwishoni
mwa juma katika ziara yake ya Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,
alipotembelea Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe na Wilaya ya Mbarali,
mkoani Mbeya katika ziara yake ya kukagua utekelezaji na maendeleo ya
miradi ya maji na upatikanaji wa huduma hiyo.
“Naagiza Halmashauri za Wilaya
zihakikishe fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji,
zisimamiwe vizuri na zitumike kufanya hivyo na zisitumike kwa miradi
mingine. Mhe. Rais Magufuli ameazimia kutatua kero ya maji nchini na
hatatutakuwa na sababu yoyote ya kutotimiza lengo hilo, na ifikikapo
mwaka 2020 tuwe tumefikia asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini
katika kutoa huduma ya maji na hili lipo ndani ya uwezo wetu”, alisema
Mhe. Lwenge.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
alisema ni wajibu wa watendaji wote wa Serikali kuwajibika ipasavyo
katika nafasi zao kila moja, kwani Serikali ya Awamu ya Tano ni ya
vitendo na si maneno. Huku akiendelea kusisitiza suala la maendeleo ya
Sekta ya Maji ni shirikishi kati ya Serikali na wananchi, na si Serikali
pekee ili kuhakikisha tatizo la maji linapatiwa ufumbuzi kwa haraka na
mafanikio.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Njombe,
Dr. Rehema Nchimbi amemuhakikishia Mhe. Lwenge kuwa wataiunga mkono
Serikali kwa kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kutunza mazingira na
vyanzo vya maji, ili rasilimali hiyo iwepo ya kutosha kwa miaka mingi
ijayo na maendeleo ya sekta hiyo yawe endelevu. Dr. Nchimbi alisema
watafanya jitihada za kumaliza changamoto za shughuli za kibinadamu
zinazoendana kinyume na Sera na Sheria za Mazingira na Maji nchini.
Katika ziara yake hiyo Mhe.
Lwenge aliweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji wa vijiji cha
Peruhanda, Wilaya ya Njombe na Ubampa, Kata ya Ubaruku, Wilaya ya
Mbarali, ikiwa ni kati ya miradi 1,800 inayotekelezwa na Serikali
kitaifa na kati ya miradi hiyo, 1,200 ikiwa imekamilika.
Tags
HABARI KITAIFA