Miaka 10 baada ya usiku wa maumivu kwa klabu ya Arsenal pale Stade De
France walipofungwa na FC Barcelona katika fainali yao ya kwanza kabisa
katika michuano ya Champions, kumbukumbu ya siku hiyo bado inamuandama
gwiji wa soka wa klabu ya Gunners Thierry Henry.
Fainali ya 2006 ya Champions League

Henry alikuwa ni moja ya kivutio kikubwa katika mchezo huo wa fainali katika ya Arsenal vs Barcelona, mchezo ambao ‘Titi’ na wenzake wa Gunners walipoteza mechi hiyona wakatalunya wakabeba uchampion wa ulaya kwa mara ya pili. Henry ambaye sasa ana umri wa miaka 38, anaeleza kwamba hakuna siku inayopita ambayo hakumbuki kilichojiri kwenye mchezo huo, pamoja na mengineyo lakini moja ya sababu za kuwa na kumbukumbu nyingi za mchezo huo ni kwasababu ulifanyika jijini Paris mahala ambapo kuna ndugu na marafiki zake wengi ambao walienda kuuangalia mchezo huo katika dimba la Stade de France.
ARSENAL VS BARCELONA 2016
Kuelekea mchezo wa raundi ya 16 bora ya michuano ya ulaya, Thierry Henry ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Arsenal pia aliwahi kuitumikia FC Barcelona – kesho ataangalia mechi hiyo huku moyo wake ukiwa umegawanyika.
Henry
anasema anaipa nafasi Barca kufuzu kuelekea robo fainali, ingawa
anasisitiza haitokuwa mechi rahisi kwa upande wowote. Kwa maoni ya Henry
ni lazima kesho Gunners wapate matokeo mazuri ndani ya Emirates: “Ikiwa
wanataka kwenda Nou Camp huku wakiwa na nafasi lazima wapate matokeo
nyumbani. Naamini Arsenal kesho watacheza kama walivyocheza na Bayern
katika hatua ya makundi – kuzuia sana kushambulia kwa counter attacks,
kwa sababu sio rahisi kukaa muda mwingi na mpira unapocheza na Barca.”
Fainali ya 2006 ya Champions League
Henry alikuwa ni moja ya kivutio kikubwa katika mchezo huo wa fainali katika ya Arsenal vs Barcelona, mchezo ambao ‘Titi’ na wenzake wa Gunners walipoteza mechi hiyona wakatalunya wakabeba uchampion wa ulaya kwa mara ya pili. Henry ambaye sasa ana umri wa miaka 38, anaeleza kwamba hakuna siku inayopita ambayo hakumbuki kilichojiri kwenye mchezo huo, pamoja na mengineyo lakini moja ya sababu za kuwa na kumbukumbu nyingi za mchezo huo ni kwasababu ulifanyika jijini Paris mahala ambapo kuna ndugu na marafiki zake wengi ambao walienda kuuangalia mchezo huo katika dimba la Stade de France.
ARSENAL VS BARCELONA 2016
Kuelekea mchezo wa raundi ya 16 bora ya michuano ya ulaya, Thierry Henry ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Arsenal pia aliwahi kuitumikia FC Barcelona – kesho ataangalia mechi hiyo huku moyo wake ukiwa umegawanyika.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA