Meli ya kubwa iliyoegemea upande
mmoja inakaribia kufika katika pwani ya Ufaransa, maafisa wa bahari
wanasema, ingawa kuna matumaini ya kuiokoa kabla ya kuzama.
Meli
hiyo kwa jina Modern Express ambayo, imesajiliwa Panama, ilianza kulala
upande mmoja Jumanne baada ya kutokea kwa hitilafu za kimitambo.Mabaharia wote 22 wameondolewa kutoka kwenye meli hiyo.
Juhudi za kuisimamisha zimefeli, lakini maafisa wanasema jaribio jingine litafanywa leo Jumatatu.
Juhudi za leo zikishindikana, basi meli hiyo itagonga pwani ya Ufaransa kati ya Jumatatu usiku na Jumanne asubuhi.
Hali mbaya ya hewa ilitatiza juhudi za uokoaji Jumapili.
Meli hiyo imebeba tani 3,600 za mbao na mashine kadha za uchimbaji, na imeinama kwa pembe ya kati ya nyuzi 40 na 50.
Ina tani 33 za mafuta.
Tags
KIMATAIFA