Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akihutubia wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha
Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza
mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000
na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
…………………………………………………………………………
Na Magreth Kinabo –MAELEZO
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,Mama Janeth Magufuli ameziomba na kuzimahamasisha taasisi
za Serikali na zisizo za Serikali kushirikiana na Serikali kutatua
changamoto mbalimbali zinazozikabili Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu
Walemavu Wasiojiweza kijulikanacho kwa jina la Nunge,viwemo vingine.
Aidha alisema vituo hivyo jumla vipo 17, katika maeneo mbalimbali nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mama
Magufuli wakati alipotembelea makazi hayo yaliyoko Kigamboni eneo la
Vijibweni jijini Dares Salaam, ambapo alisema changamoto
wanazokabiliana nazo amezisikia na na aliwaahidi kuwa atashirikiana na
wadau wote kuzitafutia majibu yake.
Mama Magufuli alizitaja baadhi ya
changamoto hizo, ni kuwa uchakavu wa miundombinu, uhaba wa rasilimali
fedha na watu, pamoja na maslahi duni ya watoa huduma, upungufu wa
vitendea kazi na huduma za jamii, pamoja na uvamizi wa eneo la kituo.
Aidha Mama Magufuli alimwomba Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema kulishughulikia taizo la uvamizi wa
eneo hilo na kulitafutia ufumbuzi.
“ Natumainni zawadi tuliyoileta
ni ndogo na haiwezi kumaliza matatizo yote mliyonayo. Lakini ni
matumaini yangu kuwa zawadi hii inaweza kuwa chachu ya kuhamsha hamasa
ya watu na vikundi vingine kujitoa kusaidia watu wasiojiweza. Ni imani
yangu kuwa endapo watu wote tutajitoa kwa dhati tutaweza kuwahudumia
wazee na watu wasiojiweza na hivyo kuwapunguzia makali ya maisha .
Tukumbuke ‘kutoa ni moyo na si utajiri’ na kwamba “sisi sote ni wazee na
walemavu watarajiwa”.
Aliongeza kwamba ni dhahiri kuwa
Serikali ina wajibu mkubwa katika kuhudumia wazee na watu wasiojiweza.
Hata hivyo Serikali pekee haiwezi kumaliza matatizo yote yanayowakabili
na wazee na watu wasiojiweza.
Hivyo basi, sote kwa pamoja tunao wajibu wa kusaidia nguvu za Serikali katika kuwahudumia watu hao.
“Na kwa kutambua hilo , mimi na
wenzangu niliombatana nao tumeamua kutoa zawadi yetu ndogo kwenu.
Zawadi hiyo inajumuisha vitu vifuatavyo mchele kilo 3000, unga kilo
3000 na maharage kilo 1200. Kulingana na idadi yenu niliyopewa kila
mmoja atapewa kilo 25za mchele, kilo 25 za unga na kilo 10 za maharage.
“Nawaombeni mniruhusu pia kuchukua
nafasi hii kuwasilisha kwenu salamu nyingi kutoka kwa Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameniomba niwaarifu kuwa yupo pamoja nayi na kwamba Serikali itaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu
wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu kwa kadri ya uwezo wake,”
alisisitiza Mama Magufuli.
Mama Magufuli aliongeza kwamba
wazee na watu wasiojiweza wanahitaji upendo, kuthaminiwa
nakusaidiwa.Hivyo kipimo kimojawapo cha kupima jamii iliyostaarabika na
inayoheshimu misingi ya utu ni kuangalia namna inavyo wathamini wazee na
watu wasiojiweza.
Aliupongeza uongozi na watumishi
wote wa kituo hicho na vituo vingine nchini kwa kazi kubwa wanayoifanya
licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Temeke , Sophia Mjema alimtaka kila mwananchi kutambua kwamba bila
wazee hakuna tutakachoweza kufanya hivyo ni muhimu kuwa enzi na
kuwasaidia wazee walioko majumbani na mitaani.
“ Tuwaenzi wazee na kuwasaidia pia
hata wale walioko mitaani tuwashauri warudi majumbani ili Serikali
iweze kuwaorozesha kwa kuwa si vizuri kukaa barabarani, Serikali ya
Awamu ya Tano ya Rais Magufuli itahakikisha inawajali wazee,” alisema.
Akizungumzia kuhusu watoto wa
mitaani alisemani wajibu wa wazazi kuhakikisha wanawalea watoto wao
vizuri ili wasikilimbile mitaani kwa kuwa watoto ni taifa la kesho.
Naye Mwenyekiti wa wazee wa makazi
hayo, Anthony Kikongoti alimshukuru Mama Magufuli kwa niaba ya
wenzake, kwa kuanza ziara yake ya kwanza ya kutembelea kituo hicho
,ambapo alimwomba apeleke salamu zao kwa baba yao ambaye ni Rais
Magufuli kuwa wanasema asante.
“Huu ni mwaka wa wanyonge dini zote tumwombee kwa pamoja ili aweze kuendelea kupunguza makali ya maisha,” alisema.
Afisa Mfawidhi wa kituo hicho,
Ojuku Mgedzi alisema wanahitaji bajeti ya kutosha ya kuendesha shughuli
mbalimbali, watumishi 42 , wakiwemo walinzi, kwa kuwa waliopo sasa ni
29 na hawatoshi.
Alisema eneo hilo lina hekari 50.8 na nusu ya eneo hilo limevamiwa.
Mgedzi alisema kituo hicho kina idadi yawakazi 112, ambapo alimkabidhi Mama Magufuli orodha ya idadi ya watu hao.
Tags
HABARI KITAIFA