Ndugu zangu,
Michangomingine
ya fedha imetoka kwa wadau wa Mjengwablog kwa kutuma kwa njia ya simu.
Siku ya Alhamisi niliongea kwenye Nuru FM na Ebony FM kuhusu wazo la
mtandao huu kukusanya misaada kwa wahanga wa mafuriko Pawaga.
Mwitikio umekuwa wa kunishangaza
hata mimi mwenyekiti wenu. Kwa fedha zilizochangwa taslimu na njia ya
simu tumeweza hata kununulia magodoro 20. Miongoni mwa vilivyokusanywa
kutoka kwa wana-Iringa wasamaria wema ni mahema 9 yenye ubora mkubwa.
Nimevutiwa pia na wanafunzi an
viongozi wa Kimarekani kutoka Programu ya CIEE niliokutana nao majuzi
ambao nao walipata taarifa hizo na wamechangia shilingi laki tatu fedha
taslimu.
Hakika, mwitikio chanya ulilazimu utafutwe usafiri wa lori kwenda Pawaga hiyo kesho.
Shukran za pekee kabisa kwa
kijana mwana-Iringa na mtaalamu wa masuala ya transport na logistics,
Ahmed Salim ‘ Asas’ ambaye amefanya jitihada za kuhakikisha
vilivyokusanywa na wana-Iringa vinafika Pawaga kesho.
Leo, Jumamosi, Feb 20, nitakwenda
Pawaga na kwa vile viongozi wakuu wa Mkoa watakuwa Pawaga, basi,
nitakabidhi misaada hiyo kwao ili nao wakabidhi kwa wahusika.
Shukran nyingi kwenu nyote mliounga mkono jitihada hizi na ambao bado mnaendelea kuchangia.
Kwa mwanadamu, kinachoangaliwa ni
moyo wako, na si ukubwa wa unachotoa. Hata moyo wako ukiguswa tu kwa
yaliyowapata ndugu zetu wa Pawaga ni faraja kwa walioathirika.
Maggid,
Iringa.
Tags
HABARI KITAIFA