BANDA MEDIA BLOG

PEP GUARDIOLA ASAINI MIAKA MITATU KUIFUNDISHA MANCHESTER CITY

Pep Guardiola
                                                                                                    Manuel Pellegrini. 

Hatimaye klabu ya soka ya Manchester City imeingia mkataba wa miaka 3 na kocha Pep Guardiola ili aifundishe timu hiyo inayoshiriki ligi kuu England. 

Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu kukinoa kikosi hicho baada ya kocha wa sasa Manuel Pellegrini kusema ataachana na timu hiyo baada ya kukamilika kwa msimu wa ligi kuu nchini humo mwishoni mwa msimu huu. 

Kutua kwa kocha huyo Etihad kunamaliza uvumi wa muda mrefu kwamba alikuwa katika harakati za kwenda kuifundisha City pindi atakapoachana na timu yake ya sasa Bayern Munich ya nchini Ujerumani.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG