Baadhi ya mashabiki wa Simba wamekuwa wakitoa lawama kwa beki wa kulia wa Simba Hassan Kassy baada ya beki huyo kurudisha mpira kwa golikipa wake mpira ambao ulinaswa na mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma kisha kupasia kamba.
Kessy anapaswa kulaumiwa kwa kupiga pasi fupi kwa golikipa wake ambayo ilinaswa na Ngoma ?
Haya hapa ni maneno ya mchambuzi wa soka Shaffih Dauda kuhusiana na tukio hilo ambalo lilizaa goli la kwanza kwa Yanga.
Simlamu Kessy kumrudishia mpira golikipa wake, namsifia sana Ngoma kwasababu unapokuwa uwanjani ukiwa kama striker lazima ujue beki wa imu pinzani anafanya nini. Ngoma alihisi Kessy atarudisha mpira kwa golikipa wake, akaenda akawahi kabla kipa hajaufikia mpira akampiga chenga kipa akafunga.
Kessy alipiga pasi ambayo kama Ngoma asingeuwahi kipa angeucheza na kama angeupiga mpira ule kwa nguvu, mpira ungemsumbua golikipa kuu-contral kwahiyo ndiyo maana aliupiga mpira kwa kasi ile ili kipa wake aucheze kwa ku-relax lakini wakati huo hakujua Ngoma alikuwa umbali gani.
Tags
MICHEZO KITAIFA