Mtendaji
Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kulia) akitoa ufafanuzi kwa
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird
aliyetembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo, Katikati ni Afisa Mwandamizi
wa Masuala ya Kisekta wa Benki ya Dunia Bw. Waleed Maliki.
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akimfafanulia jambo
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (kushoto)
alipotembelea banda la maonesho la Idara ya Malalamiko na Maadili la
Mahakama katika viwanja vya Mnazi Mmmoja leo.
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kushoto) akionesha ugeni kutoka
Benki ya Dunia nchini Tanzania michoro ya majengo mapya ya Mahakama
yanayoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini . Kutoka kulia
ni Bw. Larbi George Addo kutoka Benki ya Dunia akifuatiwa na
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (wa pili
kutoka kulia) na Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Kisekta wa Benki hiyo
Bw. Waleed Maliki.
Afisa
Magereza kutoka Jeshi la Magereza jijini Dar es salaam, Rose Odemba
(kulia) akitoa Ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini
Tanzania Bi. Bella Bird (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw.
Hussein Katanga (kulia) kuhusu Utaratibu wa kuwaachia wafungwa kwa
masharti baada ya kutumikia 1/3 ya vifungo vyao magerezani (PAROLE)
walipotembelea banda la Maonesho la Jeshi la Magereza katika viwanja vya
Mnazi mmoja leo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Utawala Mahakama ya Tanzania Bi. Wanyanda Philip Kutta
akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi.
Bella Bird (kulia) alipotembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini
Dar es salaam.
Baadhi
ya Wananchi waliotembelea mabanda ya maonesho ya Wiki ya Sheria nchini
katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakiendelea kupatiwa
msaada wa kisheria katika masuala mbalimbali.
Baadhi
ya Wananchi waliotembelea mabanda ya maonesho ya Wiki ya Sheria nchini
katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakiendelea kupatiwa
msaada wa kisheria katika masuala mbalimbali. Picha na Aron Msigwa –
MAELEZO.