Southampton itakuwa bila ya kiungo wake mashuhuri Victor Wanyama kwa wiki sita baada ya FA kuthibitisha kwamba kadi nyekundu dhidi ya West Ham inamfanya kufungiwa michezo mitano.
Hii ni mara ya tatu kwa Mkenya huyo mwenye miaka 24 kutolewa nje msimu huu, hivyo michezo mitatu aliyofungiwa na miwili ambayo inatokana na adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa inakamilisha michezo mitano.
Wanyama alipewa kadi hiyo baada ya kumchezea rafu mbaya kiungo mshambuliaji wa West Ham Mfaransa Dimitri Payet.
Wanyama alitolewa nje baada ya kupewa kadi mbili za njano katika mchezo dhidi ya Bournemouth mwezi November mwaka jana, vivyo hivyo kwenye mchezo dhidi ya Norwich mwanzoni kabisa mwa mwezi January.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA