Baada ya ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchukua ubingwa wa Afrika kwa wachezazaji wa ndani CHAN hiyo inadhihirisha moja kwa moja kwamba ligi ya Congo DR ni bora na ina ushindani mkubwa ndiyomaana wachezaji waliounda timu ya taifa kutoka kwenye ligi hiyo wameweza kufanya vizuri na kuchukua ubingwa wa Afrika.
Mtandao huu umefanya mazungumzo na Thomas Ulimwengu anayekipiga kwenye timu ya TP Mazembe inayoshiriki ligi ya nchini Congo DR. Ulimwengu anasema hashangazwi na timu ya taifa ya Congo DR kufanya vizuri kwenye mashindano ya Afrika kwasababu inaundwa na wachezaji wanaocheza ligi yenye changamoto na ushindani mkubwa.
Shaffihdauda.co.tz: Tunaomba utupe maelezo namna ligi ya Congo DR inavyoendeshwa na ushindani uliopo kwenye ligi hiyo na namna ambavyo ushindani huo unavyopelekea kupata wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao wakiungana wanapata timu ya taifa iliyo bora
Ulimwengu: Ligi inaushindani mkubwa sana ndiyo maana mtu hata kupata namba kwenye timu inabidi ufanye kazi sana kwasababu huku watu wanapambana sana kila timu inataka ikiwa kwao ipate ushindi yani hakuna timu ambayo inakuwa nyepesi bila kujali uwanja gani nyumbani au ugenini. Ligi ya huku ni nzuri sana. Sishangai kuona timu ya Congo DR ikifanya vizuri kwenye michuano ya Afrika kwasababu inajengwa na wachezaji wanaocheza ligi bora.
Shaffihdauda.co.tz: Jana mlicheza na timmu gani na matokeo ya mechi yalikuwaje, je ulipata nafasi ya kucheza kwenye mcechi hiyo?
Ulimwengu: Jana tulicheza na timu inaitwa Lubumbashi Sports na tulishinda kwa magoli 5 na nilikuwepo kwenye timu.
Timu ya taifa ya Congo DR ilishinda kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na kunyakua kitita cha dola za kimarekani 750,000 baada ya kufanikiwa kuibanjua timu ya Mali kwa bao 3-0.
Congo DR imechukua ndoo mbele ya timu zenye majina makubwa barani Afrika kama Cameroon, Ivory Coast na Mali. Wakati huo ikiwa ni mara ya pili mfululizo kushinda kombe hilo ambapo ilifanya hivyo pia mwaka 2009.
KWA HISANI YA SHAFFI DAUDA
Tags
MICHEZO KITAIFA