BANDA MEDIA BLOG

Fastjet yaongeza safari Dar es Salaam – Nairobi


 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                 ………………………………………………………………..
Dar es Salaam, Machi 15, 2016 – Shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, Fastjet Tanzania limeongeza
idadi ya safari zake  kwenye njia yake ya Dar es Salaam  na Nairobi ikiwa ni mwitikIo  mkubwa kwa mahitaji ya abiria.
Kuanzia Machi 21 fastjet itakuwa inafanya safari zake mara mbili kwa siku kwenda na kurudi  kati ya miji hiyo miwili  kila siku
ndani ya wiki na hivyo kufanya safari zake  kuwa ni 28 kwa wiki kati ya Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na Uwanja wa Kimataifa wa  Jomo Kenyatta  jijini Nairobi.
Shirika hilo ambalo hadi sasa  linafanya safari moja kila siku  kati ya miji hiyo miwili, limeongeza masafa
yake ya kuruka  ili kuwapatia abiria huduma nzuri nyakati za asubuhi na jioni.
Kwenye safari ya asubuhi, ndege itakuwa inaondoka Dar es Salaam saa 12.00 na kutua Nairobi saa 1.20. Aidha, safari ya
kurudi itaanza saa 1.50 na itatua Dar es Salaam saa 3.15.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG