BANDA MEDIA BLOG

PROF. MBARAWA AKAGUA KIVUKO CHA MV. MALAGARASI, TTCL, POSTA NA KIWANJA CHA NDEGE MKOANI KIGOMA.


B1Muonekano wa kivuko cha MV. Malagarasi kilichopo katika eneo la Ilagala mkoani Kigoma. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100, magari sita na tani 50 kwa wakati mmoja.
B2Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto), akipata maelezo ya kivuko cha MV. Malagarasi kutoka kwa Msimamizi wa Kivuko hicho kabla ya kukikagua. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani kigoma Eng. Narcis Choma na Wa pili kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe.
B3Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuka katika Kivuko cha MV. Malagarasi mara baada ya kukikagua na kuona namna ya kivuko hicho kinavyofanya kazi.

B4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akioneshwa vifaa vya uokoaji katika kivuko cha MV. Malagarasi.
B5Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akijadiliana jambo na mmoja wa abiria wa Kivuko cha MV. Malagarasi.
B6Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS, mkoani kigoma Eng. Narcis Choma (wa tatu kushoto) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), barabara ya Simbo-Kalya yenye urefu wa zaidi ya Km 200 Kusini mwa Ziwa Tanganyika itakayoanza kujengwa hivi karibuni wilayani Uvinza mkoani Kigoma.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG