…………………………………………………………………………………………………
-Zaidi ya wananchi 3,000 wanufaika nao
Utekelezaji wa mpango wa kufanya
kazi kwa kushirikiana na wakulima wadogo wadogo ujulikanao kama Go
Farming ambao umeanza kutekelezwa na kampuni ya TBL Group kwa wakulima
wa zao la Shahiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania umesaidia kuongeza
ajira ikiwemo kuboresha maisha ya wakulima.
Afisa Mwandamizi wa TBL Group
anayesimamia mpango huo Bw.Optat Morrice amesema jana mjini Arusha kuwa
mpango wa Go Farming awamu ya kwanza unatekelezwa katika mikoa ya
Arusha na Kilimanjaro mbali na wakulima unanufaisha watanzania zaidi ya
3,000 wanaojipatia ajira katika utekelezaji wake.
Aliyataja makundi ya wawaonufaika
na mpango huu kuwa ni vibarua wanaofanya kazi mashambani kwa kupuliza
dawa mashambani,madereva wa matrekta wanaolima mashamba na
kuvuna,vibarua wa kupakia mazao na kuyashusha,wasafirishaji na
watengenezaji na magunia ya kupakia mazao.
Alisema Mbali na wanaonufaika
katika hatua mbalimbali za utekelezaji wakulima wa zao la Shahiri
katika mikoa ya Kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro tayari wameanza
kuonja matunda ya ushirikiano huu kwa kuwa wanawezeshwa kuendesha kilimo
cha kisasa,kupatiwa pembejeo,mbegu na wataalamu wa kutoa ushauri na
wanakuwa na soko la uhakika kwa ajili ya kuuza mazao yao,hali ambayo
imebadilisha hali zao za maisha kuwa bora.
Morrice alisema lengo kubwa la
mpango huu ni kuinua maisha ya wakulima wadogowadogo,kuongeza kasi ya
kukua uchumi na kujenga mfumo mzuri na endelevu wa kupata malighafi kwa
ajili ya viwanda kampuni mama ya TBL Group ya SABMiller vilivyopo
kwenye nchi mbalimbali barani Afrika
“Mpango wa Go Farming haulengi
kunufaisha wakulima wa Shahiri pekee bali pia wa mazao mengine kama
mtama na mihogo na katika siku za usoni wakulima wa zao la mahindi
watawezeshwa pia na inategemewa hadi kufikia mwaka 2020 zaidi ya
wakulima nusu milioni watakuwa wamewezeshwa sehemu mbalimbali duniani
ambako kampuni imewekeza na mamilioni ya wananchi watajipatia riziki
kutokana na kufanya kazi za utekelezaji wake”.Alisema Morrice.
Aliongeza kuwa matarajio ya
mafanikio ya mpango huu katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020
yanaonyesha kukua kwa asilimia 44 katika nchi 10 ambako umeanza
kutekelezwa na inakadiriwa kuwepo ongezeko la uzalishaji wa mazao kutoka
tani 300,000 kufikia zaidi ya tani 600,000.
Mpango huu wa kampuni kutegemea
kupata malighafi kutoka hapa nchini umeungwa mkono na serikali za nchi
mbalimbali ikiwemo Tanzania kwa kuwa unalenga kuinua hali za maisha za
wananchi hasa wakulima ambao wana hali duni,hali hii imepelekea baadhi
ya nchi kuipunguzia kodi ya zuio kampuni inapofanya uzalishaji kwa
malighafi zilizonunuliwa ndani ya nchi .
Hivi karibuni Kamati ya Bunge ya
Viwanda,Biashara ya Mazingira ilipata fursa ya kutembelea wakulima wa
zao la Shahiri wanaoshirkiana na TBL Group na baadhi ya wajumbe wa
kamati hii walipongeza mpango huu wa kushirikiana na wakulima kuwa
utaweza kuinua sekta ya kilimo nchini kwa haraka na kuboresha maisha ya
wakulima.
Huu ni mfano wa uwekezaji wenye
faida kwa watanzania kwa kuwa unaeleta mabadiliko kwenye jamii na
kubadilisha maisha ya wananchi wengi kuwa bora.
Tags
HABARI KITAIFA