BANDA MEDIA BLOG

zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa Wah. Wabunge lafanyika Dodoma

kub2Mh. Saed Kubenea akisaidiwa na Afisa Usajili Bw. Surera kuchukua alama za vidole wakati wa hatua ya uchukuaji alama za kibaiolojia.

kub3Dr. Harrison Mwakyembe (Mb) akisaidiwa kujaza fomu na Meneja Usajili Vitambulisho vya Taifa, Bi. Julian Mafuru
…………………………………………………………………………………………..
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), imeanza kusajili Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; wakati wakiendelea na kikao cha Bajeti
Katika Usajili huo NIDA inategemea kusajili wabunge wote ambao hawakuwahi kusajiliwa awali na kupata vitambulisho vya Taifa, pamoja na kugawa vitambulisho
Wabunge wameonyesha mwamko mkubwa katika kutumia fursa hii adhimu, kwa kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari wa mbele kutimiza haki yao ya kikatiba ya kusajiliwa na kupata kitambulisho cha Taifa; ambacho kimekuwa na faida nyingi kiuchumi, kijamii na kisiasa
Mpaka sasa NIDA imeshatoa zaidi ya  vitambulisho zaidi ya milioni 2.5 na kwa sasa NIDA iko mbioni kuanza usajili kwa kutumia mtaji wa taarifa toka NEC ambapo zaidi ya wananchi milioni 22 watasajiliwa na kupewa namba ya utambulisho ili kuanza matumizi mbalimbali

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG