…………………………………………………………………………………………………..
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga
amemuagiza Mkandarasi anayejenga Barabara ya Dodoma –Mayamaya yenye
urefu wa KM 43.65 kumalizia kipande cha barabara ya kutoka Dodoma hadi
Msalato yenye urefu wa KM 8 ifikapo Oktoba mwaka huu.
Eng. Nyamhanga ametoa agizo hilo
Mkoani Dodoma alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma –Mayamaya
(KM 43.65), Mayamaya –Mela –Mela –Bonga (KM 188.15) ambapo ujenzi wake
kwa kiwango cha lami unaendelea.
“Hakikisheni mnakamilisha ujenzi
wa kipande hiki cha KM 8 kutoka Dodoma hadi Msalato mapema kabla ya
Oktoba mwaka huu”. amesema Eng. Nyamhanga.
Aidha, Eng. Nyamhanga amewataka
Makandarasi wote wanaotekelea Miradi ya Ujenzi wa Barabara nchini
kuongeza kasi ya ujenzi ili kuweza kukamilisha ujenzi wa barabara hizo
kwa wakati ili zianze kutumika na kuleta maendeleo kwa wananchi.
Amesema kuwa barabara hizi ni
Kiungo muhimu cha Miundombinu ya Barabara Tanzania kwani inaunganisha
mikoa maarufu ya Kilimo ya Nyanda za juu kusini, Nyanda ya kati na
Nyanda za kaskazini za mikoa ya Manyara na Arusha na pia ni kiungo kikuu
kwenda nchi za SADC kupitia Dodoma.
Eng. Nyamhanga ameongeza kuwa
Serikali kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) itaendelea
kusimamia Ujenzi wa barabara hizo ili kuhakikisha zinajengwa kwa ubora
unaotakiwaa kulingana na thamani ya fedha ili ziweze kudumu kwa muda
mrefu.
“Sisi kwa upande wa Serikali
kupitia wakala wetu TANROADS tutahakikisha barabara hizi zinajengwa kwa
ubora unaotakiwa ili zidumu kwa muda mrefu”. amesisitiza Eng.Nyamhanga.
Aidha, Eng. Nyamhanga amewaomba
wakazi walio karibu na Miradi hiyo ya ujenzi wa Barabara hizo
kushirikina na Makandarasi kwa kulinda vifaa vinavyotumika kwa ajili ya
ujenzi kwani barabara hizo zinajengwa kwa faida na matumizi ya wananchi
wote.
“Serikali inajenga barabara hizi
kwa ajili ya wananchi wote hivyo ni vema mkashirikiana na Makandarasi
wetu kwa kutunza vifaa vya ujenzi”.amesisitiza Eng. Nyamhanga.
Naye Mkandarasi wa kampuni ya
Sinohydro Coropration anayejenga sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya
yenye urefu wa (KM 43.65) Eng. Zeng Yun amemuhakikishia Katibu mkuu huyo
kuwa ujenzi wa Barabara hiyo utakamilika kwa wakati uliopangwa.
Barabara ya Dodoma –Mayamaya,
Mayamaya –Mela-Bonga yenye urefu wa (KM 188.15) ni sehemu ya Barabara ya
Kuu ya Kaskazini (The great North Road) kutoka Iringa kwenda Arusha
kupitia Mikoa ya Dodoma na Manyara.
Tags
HABARI KITAIFA