FAINALI ZA NBA, GOLDEN STATE WARRIORS YAICHAPA CAVALIERS MCHEZO WA KWANZA.
byJohn Banda-
0
Hii ni fainali ya sita mfululizo mchezaji wa klabu ya Cleveland
Cvaliers, Lebron James au maarufu kama King James anacheza. Ameweka
rekodi ya kuingia kwenye kila orodha ya kila kumi bora ya utoaji pasi,
kufunga pointi nyingi, kudaka rebound na kupokonya mipira katika hatua
ya mtoano ya NBA yaani post season.
Fainali ya mwaka huu ni marudio ya fainali zilizopita ambapo Golden
State Warriors walitwaa ubingwa huku Lebron akiwa anacheza bila
wachezaji wawili muhimu ambao ndio hukamilisha ile Big Three ya Cavs
ambao ni Kyrie Irving aliyeumia mchezo wa kwanza wa fainali hizo na
Kevin Love aliyekuwa kaumia wakati msimu ukiendelea.
Stephen Curry na Golden State Warriors walipitia njia ambayo wengi
waliamini walikuwa wameshaondolewa baada ya kuwa nyuma kwa michezo 3-1
dhidi ya Oklahoma City Thunder. Kabla ya kutoka nyumba na kuibuka na
ushindi wa michezo 4-3 huku Lebron na Cavs wakiifumua Toronto Raptors
4-2 katika fainali ya Mashariki.
Katika mchezo wa kwanza Alfajiri ya leo Warriors wameibuka na ushindi
wa vikapu 89-104. Tofauti na ilivyozoeleka sio Stephen Curry wala Klay
Thompson ambao ndio wachezaji wanaoongoza kufunga pointi nyngi zaidi
katika kikosi cha Warriors waliokuwa vinara wa pointi leo.
Curry alikuwa na usiku mbovu kwani alipata mitupo 4 peke yake kati ya
15 na kumaliza na pointi 11, huku Klay Thompson akimaliza na pointi 9
na kufanya watu hawa kupata jumla ya pointi 20 pekee kwa mitupo
27.Lilikuwa ni benchi la Warriors lililoleta tofauti kwani mchezaji Shaun Livingston alifunga pointi zake nyingi zaidi katika maisha yake ya mpira wa kikapu katika kipindi cha mtoano. Shaun Livingston akifunga moja ya vikapu vyake mbele ya Mathew Dellavedova, Iman Shumpert na Kevin LoveShaun Livingston
alimaliza na pointi 20, huku benchi la Warriors likifunga zaidi ya
pointi 50. Iguodala aliongeza 12, Green alifunga 16, Harrison Barnes
aliyeanza mchezo kwa kumkaba Lebron alifunga 13, Leandro Barbosa akapata
mitupo yote 5 aliyojaribu na kufunga pointi 11 huku Andrew Bogut
akimaliza na pointi 10.
Kwa upande wa Cavaliers, Mchezaji Lebron James alimaliza mchezo akiwa
na pointi 23 huku akipata mitupo 9 kati ya 21 aliyojaribu. Kyrie Irving
alimaliza mchezo na pointi 26 huku Kevin Love akifunga pointi 17.
Hii inamaanisha kuwa Big Three wa Cavs walifunga pointi 66 dhidi ya
36 za Big Three wa Warriors. Lakini wachezaji wa benchi ndio walioleta
tofauti kwa kufunga wachezaji wa Warriors kufunga pointi 45 dhidi ya 10
za benchi la Cavs.
HISTORIA.
Lebron James sasa ana rekodi ya kutokushinda mchezo wowote wa kwanza
wa fainali usipochezwa katika uwanja wa nyumbani yaani timu yake ikikosa
hoe court advantage. Ana rekodi ya 0-5.
Warriors wana rekodi ya kushinda 6-2 katika michezo ya ufunguzi ya fainali za NBA.
Timu zilizofanikiwa kushinda michezo zaidi ya 65 ya msimu zina rekodi
ya kushinda mara 13 katika Fainali huku zikipoteza mara 2 pekee.
Timu zinazokuwa na MVP wa ligi zina rekodi ya kushinda mara 19 katika fainali huku zikipoteza mara 7 pekee.
Timu zilizoshinda mchezo wa kwanza wa Fainali zimekuwa na rekodi ya kuwa na asilimia 79 ya kutwaa ubingwa wa NBA.