Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akieleza jinsi Tanzania ilivyofanikiwa kuhama kutoka mfumo wa urushaji
wa matangazo ya Televisheni kutoka Analogia kwenda Digitali katika
mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za
Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(Kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel wakiwa
katika ukumbi wa mikutano leo kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu
wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China
unaofanyika Beijing nchini China.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel
(kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Star Media Tanzania Liao Lanfang
wakibadilishana mawazo leo kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu wa
ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China
unaofanyika Beijing nchini China.
Mkutano wa Ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya nchi za Afrika na China ukiendelea mjini Beijing nchini China.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba na Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa wakibadilishana mawazo leo kabla ya
kuanza kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya
nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Picha na Mpigapicha wetu