—————–
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto , imesitisha tamko la utoaji wa vyakula kwa wagonjwa
watakaolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupisha utafiti
wa kina kuhusu huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora kwa watanzania.
Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba wameamua kusitisha mpango
mpaka watapotangaza tena ili kufanya utafiti kujua kama kuna faida au
hasara kwa wananchi.
“Natoa tamko kwamba huduma hii
iliyotarajiwa kuanza hivi karibuni isitishwe mara moja ili kupisha
watafiti waweze kufanya uchunguzi kujua inawasaidia kwa kiasi gani
wananchi” alisisitiza Bi. Mwalimu.
Aidha Bi. Mwalimu amesema kwamba
huduma hiyo itatolewa kwa wagonjwa watakaolazwa hapo kwa kulipia
shilingi elfu 50 ikiwemo shilingi elfu kumi ya kumuona daktari , elfu
kumi ya kitanda na elfu 30 iliyobaki ni kwa malipo ya chakula kwa wiki.
“Huduma hii inalenga kuwasaidia
wananchi katika kuwaandalia chakula stahiki kwa wagonjwa na kupunguza
usumbufu kwa waangalizi wa wagonjwa wao kuleta vyakula hospitalini ili
kuimalisha afya zao kwa ujumla” aliongeza Bi.Mwalimu.
Tags
AFYA