Azimio hili lilipitishwa kwa
ajili ya kukumbuka mauaji ya watoto wa shule yaliyofanyika katika
kitongoji cha Soweto, Afrika ya Kusini tarehe 16 Juni, 1976. Katika
tukio hilo la kusikitisha, inakadiriwa kuwa watoto wapatao 2,000
waliuawa kikatili na utawala ulioundwa na Serikali ya Makaburu. Watoto
hawa walikuwa kwenye harakati za kudai haki yao ya msingi ya
kutokubaguliwa kutokana na rangi yao.
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa
Afrika kwa mwaka 2016 yataadhimishwa katika ngazi ya Mikoa kwa
kuzingatia taratibu za mikoa husika.
Lengo kuu la Maadhimisho ya Siku
ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 Juni, 2016, ni kuwa na siku maalum ya
kuelimisha na kuwakumbusha wazazi, walezi na wadau mbalimbali kuitikia
utekelezaji wa wajibu na majukumu yetu katika kuwapatia watoto haki zao
za msingi. Haki hizi ni pamoja na haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa,
kushiriki na kutobaguliwa. Katika siku hii watoto hupata nafasi maalum
ya kujieleza, kusikilizwa, kushiriki na kuonyesha vipaji vyao mbele ya
wazazi, walezi na jamii kwa ujumla.
Maadhimisho haya, huambatana na
kaulimbiu ambayo inalenga kuhamasisha jamii kutatua changamoto
wanazokabiliana nazo watoto wa Tanzania. Kaulimbiu ya Maadhimisho ya
Siku ya Mtoto wa Afrika 2016 ni “Ubakaji na Ulawiti kwa Watoto
Vinaepukika: Chukua Hatua Kumlinda Mtoto”.
Ni matarajio yangu kuwa kila
mwananchi atashiriki maadhimisho haya kwa kuchukua hatua thabiti za
kuwalinda watoto katika jamii zetu.
- Nkinga
KATIBU MKUU
10/6/2016
Tags
HABARI KITAIFA