Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza katika hafla ya
kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza hii leo, Julai
04,2016 katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Na BMG
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka wakuu wapya wa Wilaya za
Mkoa huo kuhakikisha wanashirikiana na kamati za ulinzi na usalama
pamoja na wananchi kwenye wilaya hizo ili kukomesha mauaji dhidi ya watu
wenye
ulemavu wa ngozi na vikongwe yanayochangiwa na imani potofu za kishirikina.
ulemavu wa ngozi na vikongwe yanayochangiwa na imani potofu za kishirikina.
Amesema
mkoa huo umejipanga vyema kuhakikisha matukio hayo yanakuwa historia
kwa kuwa hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa binadamu
mwenzake kwa sababu yoyote ile.
Mkuu
huyo wa mkoa amewapa mwezi mmoja wakuu hao wapya wa wilaya kumaliza
tatizo la madawati pamoja na kuwachukulia hatua watumishi hewa 1,057
waliogundulika kwenye wilaya zote za mkoa wa Mwanza.
Mongella
amewata wakuu hao wa Wilaya kuhakikisha kwamba matumizi ya dawa za
kulevya katika wilaya zao yanakomeshwa ambapo amepiga marufuku matumizi
ya shisha katika hoteli na klabu zote za muziki pamoja uchezaji wa “pool
table” na unywaji wa pombe saa za kazi huku akitanabaisha kwamba
atakaeshindwa kutekeleza maagizo hayo ni dhahiri shahiri kwamba atakuwa
ameshindwa kusimamia majukumu yake.
Aidha
Mongella amemtaka mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha kwamba hadi
ifikapo Agosti mosi mwaka huu awe amewaondoa wafanyabiashara ndogondogo
waliosambaa kwenye maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji Mwanza.
Wakuu
wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza walioapishwa, wamesema wamejipanga
vyema kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi katika Wilaya
zao ili kuhakikisha kwamba wanatekeleza vyema majukumu yao ikiwemo
kuimarisha suala la ulinzi na usalama katika jamii.
Wakuu
wapya wa Wilaya saba za Mkoa wa Mwanza walioapishwa hii leo ni Mary
Onesmo Tesha wa Nyamagana, Estomin Francis Chang’a wa Ukerewe, Hadija
Rashid Nyembo wa Magu,
Juma Samwel Sweda wa Misungwi, Emmanuel Enock Kipole wa Sengerema, Dkt.Leonard Moses Masale wa Ilemela na Mhandisi Mtemi Msafiri Simion wa Kwimba ambapo wote wamekabidhiwa vitendea kazi ikiwemo Katiba ya Tanzania pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/20.
Juma Samwel Sweda wa Misungwi, Emmanuel Enock Kipole wa Sengerema, Dkt.Leonard Moses Masale wa Ilemela na Mhandisi Mtemi Msafiri Simion wa Kwimba ambapo wote wamekabidhiwa vitendea kazi ikiwemo Katiba ya Tanzania pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/20.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mh.Emmanuel Enock Kipole (kulia), akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto).
Mkuu
wa Wilaya ya Ukerewe, Mhe.Estomin Francis Chang’a (kushoto) akiapa
mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe.Hadija Rashid Nyembo, akiapa hii leo
Tags
HABARI KITAIFA