TUME ya Sayansi
na Teknolojia (COSTECH) imeaswa kuhakikisha tafiti zinazofanywa
zijikite katika kutoa matokeo yatakayoweza kutatua matatizo ya wananchi
na kuendelea kutengeneza ajira ili kuinua kipato cha wananchi na uchumi
wetu kwa ujumla.
Wito huo
umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce
Ndalichako wakati wa kuzindua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi,
Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Katika
Kutekeleza agizo la Uchumi wa viwanda tunategemea rasilimali watu yenye
ufahamu, ujuzi, teknolojia na ubunifu ili kuzalisha kwa tija na kuhimili
ushindani wa kimataifa.
Profesa Joyce
amesema kuwa Tafiti zilenge katika kuimarisha uchumi wa viwanda zikiwa
ni muhimu katika kuinua tija na uzalishaji,
“Baadhi ya
tafiti za Kilimo zilizofanywa na taasisi zetu kama vile Chuo Kikuu cha
Sokoine zimefanikiwa kutoa matokeo mazuri. Hii inajumuisha mbegu bora
zinazoongeza mavuno kama vile mbegu za mihogo, mahindi na mpunga ambazo
zinavumilia ukame na zinaweza kukinzana na magonjwa”. Amesema Profesa
Joyce.
Aidha
amewaomba wakamilishe mapema taratibu zinazohitajika ili watanzania
wengi waweze kunufaika na chanjo hizo muhimu kwa wafugaji wa kuku.
Nae Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt. Hassan
Mshinda amesema kuwa tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeweza
kupata chanjo inayozuia magonjwa ya kuku kama vile mdondo, ndui na
mafua katika chuo Kikuu cha Sokoine .
Tags
UTAFITI
