BANDA MEDIA BLOG

JERAHA HILI HUENDA LIKAMWEKA NJE YONDANI YANGA V AZAM


Kelvin Yondani
Beki kisiki wa Yanga Kelvin Patrick Yondan ‘Vidic’ akionekana kuumia jicho lake la kulia baada ya kupata dhoruba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.

Yondani aliingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Vicent Andrew ‘Dante’ ambaye pia aliumia mguu baada ya kugongana na mchezaji wa MO Bejaia.
Licha ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo, Yanga wametupwa nje ya mashindano hayo baada ya jana Medeama kuifunga TP Mazembe magoli 3-2, na hivyo kufikisha alama 8 ambazo, Yanga hawawezi kufika hata wakiwafunga Mazembe kwenye mchezo wao wa mwisho. Kwa sasa Yanga wana alama 4.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG