Raundi
ya kwanza ya ligi kuu ya England inakamilishwa na mchezo wa leo wa
London Derby baina ya Chelsea wanaowakaribisha mahasimu wao West Ham
katika dimba la Stamford Bridge.

Wachezaji wapya wa Chelsea Michy Batshuayi na N’Golo Kante wanategemewa kuanza leo usiku. Kurt Zouma anabaki kuwa nje ya uwanja kwa majeruhi ya muda mrefu.
Wachezaji wapya wa Chelsea Michy Batshuayi na N’Golo Kante wanategemewa kuanza leo usiku. Kurt Zouma anabaki kuwa nje ya uwanja kwa majeruhi ya muda mrefu.
Kocha wa West Ham Slaven Bilic amesema Dimitri Payet hatoweza kucheza mechi yote baada ya kuchelewa kurudi kwenye pre-season.
Aaron Cresswell na Manuel Lanzini watakuwa nje kutokana na majeruhi lakini Andre Ayew na Sofiane Feghouli wanaweza kuanza.
TAKWIMU ZA MCHEZO
- Chelsea hawajapoteza mchezo hata mmoja wa nyumbani dhidi ya West Ham katika mechi 10 zilizopita. Wameshinda 7 na wametoa sare 3.
- Wagonga nyundo mara mwisho kushinda Darajani ni mnamo September 2002 wakati Paolo Di Canio alipofungq goli la ushindi wa 3-2.
- CHELSEA
- Chelsea walipata jumla ya point 50 msimu uliopita – hizi ni points chache walizowahi kupata mabingwa watetezi wa Premier League.
- Endapo watashindwa kupata ushindi leo itakuwa wamecheza mechi 6 za nyumbani bila ushindi kutokea msimu uliopita – itakuwa mara ya kwanza kwa tangu walipocheza mechi 12 kutoka November 1994 na April 1995.
- The Blues wana jumla ya point 51 kutoka kwenye mechi zao za ufunguzi za Premier League, pointi hizi ni zaidi ya timu yoyote.
- Antonio Conte hajafungwa katika mechi 28 za ligi za nyumbani akiwa kocha wa klabu tangu January 2013. (W26, D2).
- Chelsea wameruhusu angalau goli moja katika kila mechi ya nyumbani tangu walipowafunga Norwich 1-0 mnamo November 2015.
West Ham United
- West Ham walimaliza nafasi ya juu zaidi kwenye ligi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.
- West Ham walipata point 15 kwenye London derbies msimu uliopita, pointi nyingi zaidi kuliko klabu yoyote ya London. Chelsea waliishia kupata point 12.
- Wagonga Nyundo wamefunga angalau goli moja katika mechi zao 13 zilizopita.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA